mwale wa fikira kwa maendeleo na haki za binadamu
"Mwale wa fikira kwa maendeleo na haki za binadamu" means "the ray for thinking for development and human rights". All of us can not be the UN general secretary, the presidents for party or country, the world richest people, however all of us can participate wealth empowering process! Mind deliverance is an appropriate and important step in the whole dream of improving the welfare and advocating for human rights in our earth!
Wednesday, July 19, 2006
Monday, March 06, 2006
Mwaka 2003 Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliingiza timu jijini Rome kwenda kufungua afisi mpya ya ubalozi wa Tanzania. Kwa Tanzania, mojawapo ya nchi nchi masikini sana ulimwenguni ambayo iliamua kujitutumua angalau angalau kukombeleza kile kidogo kilichopo na kuanza kujitangaza walau hawa jamaa wafikirie kuja kuwekeza nchini kwetu maana kama njaa iliishaingia suala lililobaki ni kumuuliza dada mkubwa mkubwa ajitume angalau tuliobaki tusife njaa na yule mdogo kabisa aweze kwenda shule huwezi ukajua labda atakuwa Kikwete wa kesho na kuhakikisha kuwa watu wengi na familia nyingi kama za kwetu ambazo zimetumia na zinaendelea kutumia rasilimali zake kwa hali na mali kujenga taifa bila kudai malipo angalau hazilali na njaa kama sisi tunavyolala! walau wazazi sijui kama tutafika na haya magonjwa ya kisasa ndio kama desturi ya siku, lakini Inshallah, Mwenyeezi Mungu tunayemwamini atasaidia saidia watoto wetu wasibanikike bila sababu ya msingi, kwani kuna vijana wa hapa kijijini kwetu waliotoka chuo kikuu na wako hapa kwa ajili ya likizo walidai kuwa eti nchi yetu ina mali nyingi ila tatizo tu ni kama huna meno (kama mimi baba yao niliyekuwa narudisha ruzuku serekali kiasi cha watanzania wengine kudai nilikuwa nalaza damu). wakaongezea kusema kuwa eti nchi yetu inajengwa na wenye moyo / vibogoyo na kuliwa na wenye meno! LOH AJABU HII!!ETI MIMI NI KIBOGOYO!
Katika kuangaza huku na kule, Tanzania (moja ya nchi masikini sana ulimwenguni - na yenye maslahi duni sana kwa watendaji wake hata ikilinganisha na nchi nyingi sana hata zile zenye vita za afrika)ikajikakamua na kuona kuwa kuwa na ubalozi jijini Rome nchini Italia kule kule anakotoka Pope na kwenye vivutio vingi vya utalii ni njia moja wapo ya kuifanya Tanzania yetu kuibuka kidedea (si unakumbuka hata wazee wenye hela nyingi zisizo na kazi wanaotafuta kuwekeza wa Mafia ndio kwao? ). Ombi la mshiko wa shilingi bilioni 3 likatolewa ili kuifanya Tanzania kupanda chati na kuwa na jengo la ubalozi Italy! wazo lilionekana la maana na la msingi sana! wananchi na wauza nyanya chungu wakalipa kodi (usiulize ni katika mazingira gani walilipa hizo kodi - lakini ni kwa staili ile ile ya kufunga mkanda na kuminya minya maslahi ya watanzania waaminifu na wajinga wasiokuwa wanasiasa!). unajua bwana kitu cha 3 Bn kina uwezo wa kumfanya mwekezaji ashtuke na kuingiza timu haraka haraka! wazo lilikuwa zuri!
Katika watu muhimu kwa mujibu wa kaka michuzi ambao Tanzania iliwatuma wahakikishe kuwa Tanzania inapiga bao kisawasawa ni balozi wa Tanzania nchini italia Prof. Costa R. Mahalu (Profesa wa sheria). Akiwa kizito wizarani Profesa Mahalu alifanya kazi na Waziri Mkapa wakati huo Wizara ya sayansi na Elimu ya juu - kipindi hiko ukitaka kupata scholarship ya serekali kusoma nje hata kama ni China ni budi na lazima uwakilishe bahasha kwa memba wa mtandao fulani ! wachilia mbali zile fununu nilizozipata mtaani za kutuma allowances marekani kwa wanafunzi maruhani. LOH AJABU HII! HIVI INAWEZEKANAJE HAYA MAMBO??
BASI kama kawaida watanzania waliokuwa mitaa ya Rome na karibu karibu (unajua tena kule ni kwa Pope na watawa wetu wanaotumikia kanisa katoliki ni wengi)
wakahamasishwa kuja kuonana na Raisi Benjamin W. Mkapa wakati amekwenda kufungua jengo na pia kushuhudia ufunguzi huo! si unajua tena Wabongo japo wamechoka choka lakini hawakatishwi tamaa na siku zote huamini katika falsafa ya bwana Miruko kuwa siku itafika tu! wakajitokeza kwa wingi kuhudhuria ufunguzi huo!
Kama ilivyo kawaida ya mambo ya protokali baada ya mheshimiwa Raisi wa awamu ya tatu kutinga kwenye jengo alisaini kitabu cha wageni! hapa najua wengi mnajua kuwa huwa ana kurasa wake fresh na anasaini woote! kama anavyoonekana pichani ni mheshimiwa Raisi wa awamu ya tatu alimwaga wino wakati Balozi Prof. Costa R. Mahalu akiwa anashuhudia kwa heshima, nidhamu na taadhima ya hali ya juu huku ameshikilia kikohozi hata kama kilikuwepo! mambo ya uwazi na ukweli hayo!
Kama kawaida baada ya shughuli basi wabongo waliotinga eneo la tukio nao wakapata fursa ya kuongea na mzee mzima Ben wakimpa uptdate za Tanzania viwanja vikali naye akiwapa moja na lengine kuhusiana na mikakati yake ya kuhakikisha kuwa uchumi unapanda na ikibidi kwa asilimia 10 kwa mwaka. (mara nyingi huwa siyapendi sana maeneo haya kwani huwa yanaongelea na kuwakilisha mitindo ya wana network na ya vijana waliokulia O'bay na Masaki- na si watanzania at large! - na mara nyingi hayawahusu vijana wenye vipawa ambao wanashindwa kuendelea na masomo ughaibuni kwa kukosa ada).
Raisi wa awamu ya tatu kama mzazi, kiongozi wa nchi na rafiki wa familia ya Mheshimiwa balozi alipata muda wa kuwa na wanafamilia hiyo na hata kupiga picha pamoja nao! Kwa kweli shughuli ile ilikuwa ni jambo la kufurahiwa na kila mtu kwa nafasi yake, kama taifa na kama familia! na kwa vijana kama hawa wakiwa na uhakika kabisa na future yao sio yu kielimu bali pia kimaisha! Kufanikiwa kuwa na wa/mzazi ambaye amefanikiwa katika nyanja zote kuanzia Elimu hadi Siasa ni jambo la kujivunia hasa kwa nchi inayohitaji kuwa na copyright ili kuishi vyema! wachilia mbali kuondoa nuksi kwa kupozi na mkuu wa nchi! we unacheza nini?
Haya tena hayawi hayawi yamekuwa mkuu wa nchi ndio huyo amebariki ufunguzi wa jengo na hapo ndio anaongea na vibosile wetu walioko huko Italia! hapa ilikuwa mwaka 2003! cha ajabu ni kwamba leo hii 2006 kwa mujibu wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serekali na Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) imeonyesha kuwa jengo lile la ubalozi lilinunuliwa kwa shilingi BILIONI MOJA TU! na sio BILIONI 3 kama ilivyodaiwa! uchunguzi ulifanywa hata kwa kumbana aliyeuza nyumba na kukiri hivyo, na kwamba hizo nyingine zimetafunwa na wataalamu! wengineo wakiwepo hapo chini na mheshimiwa Raisi wa awamu ya Tatu!. Je mheshimiwa raisi alilijua hilo? Je wale watanzania waliosafiri kuja kupiga makofi walilijua hilo? au miongoni mwa hao waheshimiwa waliopozi na Raisi ndio wahusika wenyewe? Je wale watoto waliopozi na Raisi wamekuwa wakifundishwa nini? Je ni yapi wanayarithi kwa wazazi wao? Je ni sahihi kuendelea na dhana ya kurithishana uongozi hata kama hakuna stahili? Je si wakati wa kuvunja dhana za kipumbafu ambazo hazina msaada kwa taifa letu?
Hadi makala hii inachapishwa, Balozi Profesa Costa R. Mahalu teyari ameonyesha mfano kwa kuwa balozi wa kwanza kusimamishwa kutokana na skendo hii noma la Mahalu. Heko raisi wetu JK tuko wengi nyuma yako! na hutaishiwa na watendaji! Hata ukifukuza 1,000 !! tumejua umedhamiria kujenga taifa la kisasa!
Swali lililobaki ni je! kusimamishwa inatosha? hizo bilioni mbili si bado tunazihitaji? sijui wanablogu mnasemaje? je tuzisare? Sasa kama maprofesa ndio wanaongoza kutia aibu, je kuna haja ya kuwa na PhD ili uwe mbunge au raisi? je tunasemaje kuhusu skendo ya PhD tatu zinazodaiwa kuwa ni feki zilivyoripotiwa na mwanablogu Miruko na wanakumekucha na teyari kwa kuaminiwa zimetinga katika wizara nyeti za serekali ya awamu ya nne? je mwaka huu atapona mtu kweli?
Tuesday, February 28, 2006
Wakuu wa AfrikaAfrika ni bara la ajabu sana ambapo watu hawajataka kuwa huru, uhuru mkubwa kabisa kimawazo na kuheshimu haki za raia wengine wa bara hili. Hii imefanya hata wenzetu wa magharibi kuendelea kuwa na wasiwasi kama vichwa vyetu vinafanya kazi sawasawa! Maana huonekana kama huwa tunaanza na mnazi badala ya chai asubuhi! Hii imefanya pia na wao kuanza kuchukua advantage kutupiga bao! Si mnajua asiyejua maana haambiwi maana? Wachilia mbali asiyetaka kujua maana!
Viongozi wengi wa Afrika toka zamani hadi sasa wametamani sana kuwa wafalme! Na hii ikawafanya wafikirie kuunda demokrasia ya mtindio ya Afrika! Ben Mkapa naye amekuwa ni muumini ya demokrasia ya kiafrika! Mara zote ni kosa kumpa wasaa Mzee Ben akiwa ni champion wa fasihi kwani ana uwezo wa kuwashawishi wale wa upande wa pili kuwa anachosema ni sahihi hata kama sio sahihi ! kuna vilivyo sahihi alivyowahi kuvisema lakini mara zote amekuwa akijizungumzia yeye na wale wanamaslahi waliomzunguka wengi wao wakiwa wametupwa huku na kule ulimwenguni wakila starahe 24/7!....nitatoa mfano Dr. Ben akiwa anapewa PhD ya heshima ya sheria katika chuo kikuu cha Lesotho Roma Campus aliongelea mengi moja wapo ni muundo wa demokrasia ya Afrika. (kiungo hakiunganishi lakini mkiitaka nitawatumia nakala yake, nimeihifadhi).
I also accepted the invitation because I have always wanted to come here and pay my respects and tribute to the glorious and heroic Basotho ancestry, the independence of this country and the innovativeness of its leaders and people in their PROCESS OF POLITICAL MODERNISATION. We in Tanzania followed with keen interest the evolutionary development of your constitution, the strengthening of your electoral machinery and processes, and the entrenchment of the system of democratic REPRESENTATION SUITABLE TO YOUR CIRCUMSTANCES (which circumstances? mbona hajazungumza? Kuhalalisha William na vizazi vyake wanatawala daima na sio Omari na vizazi vyake?). Je mheshimiwa raisi wa wakati huo ana uhakika kuwa alichosema hapa wana Lesotho walikifurahia? nadhani kuna haja ya kujifunza majority wanafikiria nini na wanajisikiaje badala ya kutukuza wakuu!
Democracy and good governance are universal values, but we do not have to copy, hook, line and sinker, Western democratic models developed by, and anchored in, societies that are different from ours. Universal values of democracy, human rights and good governance are not a cult; they have to be tailored to the society in question. Even in the old democracies, democratic governance systems and processes are not uniform. We can and we should have democracy and good governance with African characteristics (DEMOKRASIA YA AFRIKA INASISITIZA KUIBA KURA – AU INAKUWA IKITRANSFORM INTO MONARCHY – UFALME? Mfano Swaziland? Gabon, Uganda? Perhaps Tanzania? ).
Alipokuwa chuoni miaka ya 1960 Bwana Harry Raid alijadiliana na Marehemu lord acton “Power tends to corrupt, and absolute power tends to corrupt absolutely.” gonga hapa huyu bwana alikuja kuelewa somo baadaye sana baada ya kumaliza shule ni nini maana ya ujumbe huu!! – ni kwa namna hiyo hiyo hata bwana Githogo ambaye amejiuliza kila kukicha kabla ya kupata cheo kilichomweka kwenye nafasi ya kuibua kimbembe cha Anglo leasing huko Kenya "I have always been fascinated by the connection between corruption and politics," Githongo natumaini kama anagalikuwa kwenye darasa moja na bwana Harry Raid angenufaika zaidi! …nadhani ni zaidi ya hapo, najua alielewa kabisa labda swali la mana zaidi la kujiuliza kuwa “ni kwa nini imekupasa kuendelea kung’ang’ania madaraka – ikibidi kwa rushwa?” je kiongozi anayepatikana katika mazingira ya rushwa anatufaa? ndio suala la msingi la kujua ili kujua jinsi rushwa inavyopaliliwa! Mwanablogu Tungaraza alituibua na kimbembe cha dola milioni 3.7 (ambazo kimsingi zingekuza ufanisi katika jeshi la polisi kama sio kukabiliana na njaa au hata upungufu wa umeme) zilizopotea katika jeshi la polisi !. Kwa wakati huo huo tunamuona muhishimiwa sana mbunge na waziri mtarajiwa wa wizara nyeti ya Tanzania siku si nyingi, Bwana Omari Ali Mahita akiendelea kujihakikishia kuwa yeye ni mungu mtu ndani ya sayari Tanzania! Kwa kuuhakikishia uma kuwa kama alivyosema ataondoka kwa kustafu polisi anastaafu huyooo ndivyo itavyokuwa na kutangaza kustaafu wiki hii mwishoni. Teyari tunaona wakubwa (sio wadogo) katika jeshi la polisi teyari kama ilivyo utaratibu wa serekali zinazoongozwa na mkumborasia (sio demokrasia) kama alivyoziita bwana Nkya wameanza kumsifia kuwa amefanya mengi kwa taifa na ni mfano wa kuigwa!. Polisi wadogo wamelia kuwa jeshi limeendeswa kama idara binafsi kilio cha polisi wadogo .
Naye pia akawaasa waache kusikiliza uzabina ambao unataka kuligawa Jeshi la polisi “sijui katika makundi yapi na yapi yaliishakuwapo na yapi ambayo hayajawahi kuwepo kabla” ! Sijui kama wanajua kuwa saa yeyote anaweza kutinga The Hague, au wanataka kutuambia kuwa wao damu za watu ambazo Mahita amezimwaga bila sababu yoyote ya msingi ni jambo la kuchekewa! Mahita ni IGP ambaye amechemsha kuliko wote na ameongoza kuvunja sheria na haki za demokrasia na binadamu. Wachilia mbali tuhuma zinazomkabili za kujipatia “utajiri mchafu!” Wakati CCM ikiendelea kuwa katika njia panda juu ya njia mbadala ya “kuepusha shari” kama ilivyonukuliwa na bwana Mpinganjira shari tupu CCM hadi ikafikia kipindi bwana Chitalilo kushindwa kuvumilia na kupania kuwafukuza wabunge wa CUF kwa kuanzisha kimbembe cha Mahita Bungeni mchemsho wa Chitalilo. nadhani mkabala umekuwa ni yeye kutangaza kuwa aliomba kitambo kustaafu na raisi JK aliishalikubali hilo! ..hivyo yanayoendelea sasa ni maneno ya inzi ambayo hayamyimi simba kula windo lake. Wakati bwana Mahita akiachia ngazi kwa minyato “cut walk” na maringo mithili ya dume la twiga, hivi tunavyoongea teyari amemuaga waziri kiongozi wa Zanzibar byebye Shamsi
.
Wakati Mkuu Mahita anayoyoma kwa “cut walk” ni siku chache kwa mujibu wa bwana Michuzi raisi akihutubia wakati akifungua semina ya TAKURU alizumgumzia eneo la nne lililogubikwa na rushwa na la kufanyia kazi.....kuwa ni SIASA na akaomba TAKURU walishughulikie severely!! - SUALA HAPA NI JE ALICHOFANYA MAHITA SI SI RUSHWA? . Hapa amemwacha Mh. Raisi Kikwete na swali gumu la kujibu kuwa je anaungana na bwana Ben kuhusu matumizi mabaya ya polisi kuvunja haki za wananchi wake? Je yuko tayari kuchafua CV yake, charisma na uwezo wake kama mwanasiasa kukiri kuwa, asilimia 80 % ya wapiga kura kumpa yeye kura ni matokeo ya juhudi ya bosi wa polisi? Na pia kuona kuwa maendeleo, upendo na imani ya wananchi kwake inafunikwa kama giza?. Kwa kweli jinsi mh. Raisi atavyoujibu mtihani huu ndio dira pekee ya kuuonyesha umma kuwa amedhamiria kupambana na makunyanzi la sivyo historia itajirudia kuwa Fupa lililomshinda fisi yeye atalimudu vipi? kama alivyoandika bwana Karl Lyimo mwaka jana natafuta ukuu wamwalimu . Wakati tukiendelea na kutafakari hii je mauaji ya Sinza na uundwaji wa tume yanaweza kabisa kuwa Drama ya kufunika hili suala? Mie siongezi hapa – majibu mnayo wenyewe!
Katika hotuba yake Mheshimiwa Mkapa alivishambulia pia vyuo vikuu vya hapa nyumbani kuwa havifanyi kazi inavyotakiwa!
The oldest and biggest university in Tanzania, the University of Dar es Salaam, is situated on top of a hill overlooking the city, hence its nickname “The Hill”. This fits and reinforces the notion of intellectual aloofness that is often, rightly or wrongly, ascribed to university dons and graduates in their fancy hoods and gowns. My apprehension in addressing university communities derives from the belief that, in Africa, town and gown do not often see eye to eye.
So, I thought that since I am about to leave office, I could afford to venture into the delicate arena of relations between the town and gown in Africa. After all the people who run and manage the town were once in hoods and gowns too. – KWA NINI ANAFANYA AKITOKA IKULU? SWALI HILI PIA LINAENDA KWA DR. SALMIN AMOUR AMBAYE ANAUJADILI MUUNGANO KAMA MTAZAMAJI WA MPIRA AMBAYE HANA UWEZO WA KUFUNGA GOLI!
And I am sorry to say that most African universities, upon which we depend to produce the next generation of African leaders, do not sufficiently internalise these challenges into their curricula, research programmes and general disposition. In general terms, our academics evince the greatest inertia in this regard. In my work with the World Commission on the Social Dimension of Globalisation, and later in the Commission for Africa, and since then, I have bought and read many books and research papers on these subjects. Believe me, the contribution of African scholars, academics and researchers to such debates and literature is negligible. It is us Africans who are most adversely affected by the status quo; yet we leave it to scholars, academics and researchers from rich industrialised countries to analyse our predicament for us, and determine the agenda ahead for us. – JE ALIFANYA JUHUDI GANI KUHAKIKISHA KUWA VYUO VRETU VINAFANYA KAZI INAVYOTAKIWA? JE KWANINI ALIRUHUSU VYURA WA KIHANSI KUPELEKWA MAREKANI KUTUNZWA NA KUFANYIWA UTAFITI KITU KINACHOIGHARIMU SEREKALI HELA NYINGI? JE HATUNA WATALAMU MAPROFESA NA MAPROFESA WA ZOOLOGY HAPO UD? Hivi karibuni Raisi JK ameamrisha kurejeshwa kwa vyura wetu! chura wetu warudi
Sio kwamba nimepanda jukwaani kumshambulia Ben la hasha, ila nimekuwa na wasiwasi na miwani anayotumia kuona mambo kwenye baadhi ya maeneo. Lakini labda imetokana na kulelewa katika mfumo ambao haujawahi kumtenda ovu kama bwana Lyimo alivyofafanua, au kwa kifupi ameshinda akila mema ya nchi “Apparently, Mkapa had been in a class taught by Nyerere at Pugu Secondary School in the 1950s. Later in life, he had served in the Nyerere Administration in ROLES THAT MANY WOULD ENVY, but would FIND DIFFICULT TO LAND under the austere Mwalimu”. Mfano kama yeye akiwa serekalini hakuwahi kuulizwa kuhusu rushwa je kwanini yeye ahoji watendaji wake? Tunakumbuka alisisitiza aletewe evidence na kwa upande wa pili maana yake ni kusisitiza wafanyakazi wake wale rushwa kisayanzi zaidi? Labda wimbi hili la lawama katika maeneo Fulani Fulani ndilo limemfanya hata JK apande jukwaani na kuitetea miwani na utendaji ya serekali iliyopita kong'oli hapa.
Kupanda kwangu jukwaani ni kuja kuangalia je ni aina gain ya demokrasi tunayoitaka Afrika? Je demokrasia hukamilika pale tu shemeji anapoupata ubunge au uwaziri ? viongozi wa Afrika wakiongozwa na mwanafasihi Ben wamekuwa mbele kuwashutumu wale wa magharibi kuwa ‘wale wa magharibi huona demokrasia imekamilika pale tu upinzani ukishinda’ ! binafsi sioni mantiki ya usemi huu zaidi ya kwamba una lengo la kujitafutia legitimacy ya kupata ushindi hata pale ambapo hakukuwa na ushindi ! usemi huu una mantiki ya kusisitiza kuwa mtawala aendelee kuwa mtawala hata kama hafanyi mema kwa watu wake ! lakini tukirudi kwa hao wenzetu wa magharibi, je hatuoni mabadiliko ya mara kwa mara katika uongozi ? je hatukiri kuwa mabadiliko hayo yana maana kwa watu wake ? siko kwenye kampeni ya kudai legitimacy ya JK au AK kuwepo madarakani ila nina maana ya kuwa je kwanini ilifikia mahali utashi wa binadamu ukaonekana kuwa ndio chombo cha kufanya maamuzi ya uongozi ? na je kama utashi huo hautaenziwa kuna haja gani ya kufanya maigizo na kupoteza mamilioni ya fedha badala ya kuzipeleka katika shughuli nyengine za maendeleo ? je Mheshimiwa Mkapa alikuwa anamnyooshea kidole nani alipokuwa anasema haya ? je tunakumbuka jinsi mwanataaluma mwandishi Mheshimiwa Mkapa aliposhindwa kusubstantiate maoni yake haya katika kipindi cha hard talk na kuanza kufoka ? ni vyema tukajifunza kuwa na arguments ambazo zimelala ilipo haki – kamwe hatutawaona waandishi wa wenzetu wabaya !
Watawala wa afrika wamekuwa wakiendelea kukumbatia uchafu kwa labda kuogopa kucross line « kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyengine » au "kumfagilia mtawala mwovu "! kuna kina Omari Bongo mmoja wa viongozi aliyetawala Gabon kwa muda mrefu tu akiwa mtu mwenye mali nyingi sana na kuongoza moja ya nchi masikini sana afrika ! Labda hapa niweke mtihani « je Julius Nyerere aling’atuka au alipaswa kuachia jukwaa ? » "je ni nani anaweza akaongelea umaarufu wa mwalimu ambao angekuwa nao sasa hivi kama angeendelea kung’ang’ania madaraka ? " « je angeweza kuwa raisi bora wa wakati ule kuliko alivyokuwa Ali Mwinyi ? ». Binafsi pamoja na kufikiria kuingia kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki bado sioni ni kwa nini viongozi wameendelea kumkumbatia Museveni (pamoja na demokrasia wanayoona inayowafaa Waganda), Wamemtukuza Bakili Muluzi ambaye ameifikisha Malawi kwenye matatizo kwa kuwa mla rushwa namba moja. Miaka takribani miwili raisi mpya wa Malawi amekuwa akipigana kufa na kupona kupambana na nguvu za Muluzi ambaye alifika mahala akajipa kila chanzo cha uchumi cha malawi wachilia mbali kusajili mali zote na magari yote ya chama chake kwa jina lake, hivyo kutoa pale tu anapoabudiwa ! ni Muluzi huyo huyo ambaye aliuza « alipiga dili » mahindi ya akiba ya taifa na hivyo kuitumbukiza Malawi kwenye baa la taifa la njaa ! na baada ya hapo kama kawaida ya viongozi wetu "wanapoharibu" akarusha shutuma kwa IMF ! Lakini kwa namna ya ajabu waMalawi wakashangaa kumwona Waziri John Komba na TOT yake wakiingiza timu kumpigia kampeni kwenye kipindi chake chga pili ! yeye alipania kuwa raisi wa maisha wa Malawi !. tumemsikia Museveni akitaja taja Nyerere na CCM akiwa kwenye kujifagilia maana imedaiwa kuwa CCM ni chama imara kuliko vyote Afrika ! « mimi ninaona kuwa katiba ya AU ina haja kubadilishwa na kuainishwa waziwazi kuwa kuingilia mambo nchi ya mwezio ni ruksa ikiwa tu unatetea maslahi ya wazee- watawala na sio fukara, wanyonge, na hohe hahe wapiga kura kama kina sie ambao tuko wengi ! »
Viongozi wanaoingia ikulu kwa mazingira ya rushwa hujisahau kwani wamekuwa katika ulimwengu tofauti kabisa na wa wapiga kura wao, na ni biashara ambayo iliishaisha ! rushwa ya kisiasa nayo ina matatizo mengi sana mara nyingine hupelekea matatizo kama yaliyomkuta Bob Robert Mugabe ambaye kwangu mimi ndiye kiini cha mjadala ! labda kabla sijaendelea na mjadala huu nitanukuu mambo machache. Nitajitahidi kuangalia pande zote ili kuepuka ile dhana ya kutupa shutuma kwa «vyombo vya magharibi kuwa vinawaonea waheshimiwa sana watawala wa afrika , wao pamoja na wapendwa wao » na « pengine havitekelezi haki kwa walio wengi » !. tumeona ni jinsi gani watu wamekarabatiwa na polisi katika uchaguzi ulizopita wakati « vyombo vyetu vikikaa kimya na kupamba taarifa za uchaguzi sina uhakika ni kwa ajili ya walio wengi ? » na vyombo vya magharibi vikilaumiwa kwa « kusema ukweli pengine pia kwa manufaa ya walio wengi ?» - kwa hili sisemi sana maana kila mtanzania siku hizi amegeuka mpiga dili kwa kizungu « misheni tauni » – kutibu njaa ya muda huo na kumwachia mungu ya kesho !. kwa wasomaji wa blogu basi tusome blogu nadhani Zimbabwe inaongoza (tafuta tu kwenye blogu), ili kuacha kudai hii ni CNN na hii ni BBC, pia tuwatafute wa Zimbabwe popote walipo ili tujue ni nini hasa kinachoendelea !
Binafsi nikiwa Mtanzania niliyekuwa ndani ya yai muda mrefu nikileweshwa na historia za ukombozi wa mtu mweusi sikuwa tayari kukusolewa kwa wapigania uhuru wetu ! labda nilimwona Mukgabi kuwa ni mtu wa maana hadi nilipojua ya kwake ! umaana wa Mugabe ulikuwepo kwenye kudai uhuru na kusomesha watu wake Zimbabwe ikiwa na asilimia 85 % wasomi fanikio na kutafsiriwa ndio imekuwa pia ni hatari kwake kwani viongozi weni wa afrika hawapendi wasomi kwani wanageuka mbu na kuwanyima usingizi !
kwa taarifa tu kuhusu habari ya wakimbizi , zaidi ya robo ya wazimbabwe waliishatoroka nchini kwao na katika hao asilimia 70 % ya wasomi waliishaishia ! wakimbizi Zimbabwe . hadi mwaka jana katikati Mugabe aliisha tengeneza wakimbizi milioni 3 kwa afrika kusini peke yake!.... Hapa nilipo SA kuna wazimbabwe wengi tu kwani hadi kufika mwaka jana kati kati teyari waliishakuwepo milioni tatu ! wanakuja kuongeza namba yetu MAKWEREKWERE!
Jamani kwa wenzetu ambao labda mpo popote ulimwenguni tujitahidi kuangalia hili suala kwa undani zaidi ya kusema wazungu versus waafrika! Mmesahau Ben aliwahi kutuambia kuwa « paka ni paka tu halijali rangi? » kabla hatujafika mbali labda tusome huu uchambuzi wa Profesa Moyo ambaye naye amewahi kuwa mshauri wa Raisi Mugabe wa masuala ya adhi ambayo aliitoa pale Ethiopia. uchambuzi wa Prof.Moyo ambapo na mimi nilihudhuria. yeye bado yuko Zimbabwe na ndani ya hiyo makala amekiri kuwa kuna udhaifu katika utekelezaji wa land reforms ! alikiri kuwa kamba ilikatika katikati pale wakina Toni Blea waliposita kuendelea kufadhili mpango huo ! huu ni ukweli ! ni kwa nini lakini ? kina Blea waliwahi kusema kuwa Mugabe alikuwa anakula hela za program !! kitu ambacho mimi nakubaliana nacho ! kimsingi Mugabe alikimbilia kuwaachia watu kujigawia ardhi bada ya kugundua kuwa ilikuwa ndio agenda ya MDC kumuuliza wakati wa uchaguzi ! sawa amebakia madarakani – fact ! lakini kajenga au kabomoa ? nilitoka machozi baada ya Mheshimiwa Ben kutoa kile kilichoitwa « chilling speech » katika mkutano wa SADC na kujichukulia ujiko kama shabiki namba moja wa Mugabe !soma hapa hotuba ya Mkapa
President Benjamin Mkapa of Tanzania is an outspoken fan of Mr Mugabe and entertains the curious belief that this dictator is a "champion of democracy". In fact, if he is a "champion" of anything, it is misery, as illustrated by yesterday's figures showing that life expectancy in Zimbabwe has fallen to just 33, compared with 63 in 1988.
Kwanini nilitoka machozi? Alikuja Mzimbabwe mmoja akaniuliza “does honourable Ben Mkapa your president have children?” nikamjibu "yes indeed"! Akaniuliza tena “does he know what suffering might be?” nikamjibu “probably yes” lakini safari hii kwa woga woga nikuendelea kutafakari picha mbili za Ben, kama kiongozi wa Afrika ambapo upande mmoja anapigania maslahi ya mtu mweusi kwa kusite mfano wa Mugabe, lakini kwa wakati huo huo huficha uchafu kwenye kucha zake
Ninawajua wazimbabwe, ninaishi nao! Ninajua jinsi walivyo na mizigo ya kubeba nyumbani walipotoka! Kila mwezi wanakuja ndugu zao kutafuta dawa za mishwaki na bidhaa za matumizi nyumbani!! Ninafanya nao kazi ninawaambia siku moja ninarudi kwetu! Wananiangalia kwa macho ya huruma! Wananiuliza kama ninaweza kuja nao Tanzania! Jirani wao wazambia nao wanacheka chini chini! Eti kwacha imepanda chati – maana kuna wakati kuingia Zimbabwe ilibidi kuwa na visa! Sio sasa tena, hawana jeuri yoyote! – Je ndipo tulitaka kufika huko? Je ndio spirit ya Afrika kuunga mkono mtawala MHARIBIFU at any cost? Kama SA inaunga mkono iweje wao wanafanya land reforms kwa kufuata taratibu na wasifanye kama Mukgabi (serekali ya SA hununua ardhi kwa wakulima wa kizungu walio tayari kuuza na kuwagawia weusi – hata hivyo taarifa za kushangaza ambazo niliziona kwenye TV ni kuwa waliopewa mashamba hayo wameishaanza kukiri kushindwa kuyaendesha, na serekali ikihisi kuwa imekula wa chuya) Mimi nadhani kama nia ni kuona watu wanateseka, dhana ya Africanising the democracy si sahihi ! Hebu tufuatilie habari hii kiundani ili kujua kama wanaohusika na sakata hili la wazimbabwe ni mamisheni tauni wa mjini au raia wengi! Tujue pia Mukgabi anaishije ishije, na ni katika mazingira gani hufanya kazi zake! Kwa uchache wa muda nitaweka machache mengi mtaendelea kutafuta wenyewe! Yako mengi tu tena toka kwa wasema lolote wa MAGAZETI TANDO KAMA SISI – si lazima uende kwa wanaoitwa wasema uwongo CNN au BBC! Teyari ameibatizwa kuwa ni mfalme mugabe ni mfalme
kama Mugabe ni mwana wa Afrika, kwa nini basi ilimpasa kuwa na mali nje ya Afrika ? hii inaonyesha kuwa uwezo wake kuwa na mali nje ulienda sambamba na kufa kwa programu ya kugawa ardhi? Kwanini nasema hivyo? Mara baada ya kuanza operesheni ninayoiita “operesheni rudi ikulu” waheshimiwa wakaseeze asset zake zilizopo ulaya! wamechukua wameweka
Mugabe’s akitumia ndege ya umma kula raha “Air Zimbabwe” alifanya safari zilizoifanya Air Zimbabwe ikodi ndege nyingine na kuiingizia hasara ya zaidi ya ola milioni moja ufujaji kwa jina la raisi. katika nchi yenye njaa (watu milioni 6 wakihitaji msaada wa chakula) watu walichanganyikiwa sana kuona mhishimiwa akirudi na wapendwa wake wakiwa na makontena ya nguo na zawadi!. Mugabe hula raha za namna hii kila mara ughaibuni!
Kama viongozi wengine wa Afrika, amepuliza hela nyingi sana kwenye kujenga usalama wa taifa, kwa sasa CIO inatumia bilioni 3 zaidi! Kwa namna hiyo ameweza kuwavuruga kina Tshivangrai na kutumia mbinu za midani “kuua upinzani” kwenye MDC soma hapalakini watu bado wameshika bango kulikoni?.
Akishauriwa na mshauri wake mchemshaji Mengistu Haile Marimu ambaye ni kinara wa udikteta katika afrika (hajawahi kuwa na historia iliyompatanisha na ubinadamu) alienda kuvuruga vibanda vya watu 700,000 ka kuwaacha hao wakiwa hawana makazi! Watu hawa ilibidi wahamie karibu na penye riziki (kubanana hapo hapo). Mukgabi alikuwa ni mtu wa kwanza na pekee kunyoosha mkono kumkubali Mengistu alipozidiwa nchini kwake! Mengistu ambaye alijiita mwana wa Afrika kupinga ubepari ni Bepari mkubwa tu Zimbabwe akila raha kupitia majasho ya walipa kodi wa Zimbabwe! wasemacho ndicho watendacho?ukienda pale chini utaona stori nyingi tu kuhusu Mugabe! Picha zaidi hapa picha bloguni .
Bila aibu alijifanya kuua soo alipotembelewa na mama Profesa Tibaijuka ambaye ni mwenyekiti wa shirika la makazi la UN (HABITAT). alichokuwa anatamka ni tafauti na kilichokuwa usoni mwake kwani alikuwa anaangalia chini « Kama ni wewe sawa wewe umetumwa na Koffi Annan na sio mjinga Blair ». Kwani hajui kuwa hata Blair yumo ndani ya UN ?
Cha ajabu ni kwamba UN katika jitihadi za kuwanusuru wakazi laki saba wasio na makazi iliwapelekea mahema ! kidume huyu akaja tena akidai kuwa « Wazimbabwe hawaamini katika mahema bali nyumba » na kuutkata msaada ule akili yake iko sawa kweli?
7. Tunapoongelea sasa theluthi tatu ya wazimbabwe ni masikini kupindukia ! lakini utashangaa kuwa chakula cha misaada hutolewa kwa wanachama wa ZANU PF tu wote si ni walewale tu?
Wakati wazimbabwe wakiendelea kuteseka, bwana Mugabe ameendelea kutesa kwenye 82 na akijiita yeye ni kijana katika wazee kijana wa wazee wakati ambapo teyari ameishaanza kupoteza kumbukumbu. Alitoa kali zaidi alipomwita ofisa toka ng’ambo aje ampe kazi mpya na alipomwona ikulu akamuuliza kafuata nini ! ilibidi dada wa watu ajikaushe arudi Australia. Iliwashtua sana mawaziri ! bila aibu aliagiza majuzi kila provinve watu wachange amgalau dola za marekani elfu kumi na tano kwa ajili ya bathidei yake ! na wakati huo huo kuwa mzigo kwa wannchi kupaka rangi nyumba zao wakati hawana chochote ! huyu kawahi kuzaa kweli?
Watu mbali mabli ndani na nje ya Zimbabwe wamuishaanza kumwambia akae kushoto angalau mambo yaende kong'oli hapa . viongozi wa Afrika nao wakamtolea uvivu kuwa anachemsha gonga uonenaye akawajibu kuwa ni wajinga mugabe ajibu na akanukuliwa na mjadala na Tungaraza na akaongeza mnikome ! mnikome mwana wa mwenzenu
Hayo ni yale niliyopata nafasi kuchambua kama nukuu ndani ya siku hii baada ya kuona mjadala kwa bwana Mwandani. Miongoni mwa yasiyoandikwa hapo ni
huwa anaenda benki kuu ta zimbabwe na kuwaamuru wataalamu wacheze na figa kuonyesha kuwa uchumi hauanguki. 2003 Alifanikiwa kushusha inflation toka 600 % hadi 0 % na sasa umerudi pale pale. – sijui kwa faida ya naini ! Tunayo aina hii ya viongozi kila mahali !
alipoona mabo yanakuwa mabaya kimaisha hadi kwa jamaa zake, akanzisha Senate ili waweze kuishi ! tunavyoongea sasa hivi ni kuwa ni wale tu ambao wako kwennye circle yake wanaweza kuishi ! gari likiisha mafuta linasimama hapo hapo !
ugawaji wa mashamba haukuenda kwa walengwa, ilikuwa mbadilishani wa wakubwa weupe kwa wakubwa weusi ! watu wakafukua mabomba ya kumwagilia wakauza kama scrap ! wakachinja ng’ombe za maziwa wakala nyama, wakaendesha matrekta kwenda bar ! je tushabikie hii ilivyotokea kwa kuwa na sisi ilitukuta kama ilivyokuwa azimio la Arusha na kushabikiwa kama kawaida na mheshimiwa Mkapa ?
Fourth, we now hear a lot of stories about Zimbabwe. I am convinced that the root cause of the vilification and demonization of Zimbabwean leaders – and I am sad that some African media echo the line of the Western media – is land. You can agree with me, or you may disagree with me. But, I am convinced that all the “sins” of Zimbabwe would have been easily forgiven if they would not have dared to speedily redress the historical injustices related to land ownership in that country. And if this makes Zimbabwe a “failed state”, we have to ask why. Is Tanzania also a failed state because we want to protect the people’s basic, God-given, asset – Land? Or is it because of how we do this? Is it a question of intent or of methodology? African universities should analyse these issues and create more awareness about them among our youth, especially as to them the indignity and the injustices of colonial rule seem so distant and so unreal.
Je kama utawala wa Mugabe usingekuwa fisadi, ukafanya kazi yake inavyotakiwa kuwa, kugawa ardhi kwa wakati mwafaka, je wasingejikuta wanafuata mode ya Afrika Kusini na kuliko vamia vamia ambayo imeigiza hasara zaidi kupitia “operesheni rudi ikulu?”
Tunavyoongea kwa sasa amechukua wanajeshi wake na kuwapeleka kulima mashamba ili watu wale!!!
Kuna waheshimiwa wakiwa ndani ya chama chake na wafuasi wake waklitunga sheria za kuufagilia utawala wake, e.g. kufungia vyombo vya habari! Mmojawapo ni Prof. Jonathan Moyo. Leo hii analia kwani naye amebanika baada ya kuwa kinyume chake! JAMANI SHERIA NI MSUMENO NA HUWEKWA NA WATU!
SITAONGEZA ZAIDI LAKINI NINADHANI UMEFIKA WAKATI JEMBE LIITWE JEMBE NA SIO LEBESHI! JE TUNATAKA KUFIKIRIA KUWA NA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO HUFICHA MAOVU? SAWA HATA KAMA NI KWA FAIDA YA NANI? – JE WEWE UNGEKUWA NI MWANAZIMBABWE UNGEFANYA NINI? JE TSVANGIRAI NA WENZIE WAKIMBILIE WAPI IKIWA MFALME MUGABE AMEBANA PANDE ZOTE? JE NA SIE TUSHABIKIE KUWA TSIVANGIRAI NI KIBARAKA WA BLAIR HALI TUNAJUA KUWA NI MAZINGIRA YANALAZIMISHA KUWA HIVYO ? NA JE ATAKIMBILIA WAPI IKIWA MIMI NA WEWE TUMEPANDISHA TINTED ZETU HADI JUU?? – JE SISI NI MASHABIKI WA MAANGUKO YA ZIMBABWE NA MATESO WA RAIA ZAKE?? JE TUENDELEE NA DHANA POTOFU YA KUKUMBATIA VIONGOZI WABOVU NA WALIOJAA UBINAFSI KWA KUWA TU TULIWAPATA KWA KUTUMIA MTINDIO WA MKUMBORASIA YA AFRIKA? - JE TUTAFIKA KWELI?
Thursday, February 23, 2006
msakimark@yahoo.com
Subject:
TANZANIA ECONOMIC FORUM
Date:
Wed, 22 Feb 2006 15:48:49 -0600
From:
"Tanzania Economic Forum"
Kwa kupitia vyombo vya habari inawezekana ukawa umeona kuna kundi dogo la wabunge wa kipindi kilichopita waliokutana Dodoma tarehe 27 Desemba 2005 na kuamua kuunda Taasisi walioipa jina la “TANZANIA ECONOMIC FORUM”.
- Ndani na muongo huu nchi ilikabiliwa na misukosuko ya kisiasa baina ya vyama tofauti na ndani ya vyama vyenyewe. Kadhalika kipindi hiki kilionyesha dhamira ya serikali kujitoa katika umilikaji wa rasilimali za Taifa na udendeshaji wa uchumi. Sekta binafsi ilipewa fursa ya kushika hatamu na kununua mashirika yaliyokuwa ya umma
Juhudi za kufufua Ushirikiano wa Africa ya Mashariki pamoja na kubadilisha mfumo wa ushirikiano na nchi za kanda ya kusini mwa Afrika.
- Ni Katika kipindi hiki hatua za kisheria zilifikiwa na kuielekeza nchi yetu kwenye soko la pamoja na nchi za kanda ya Africa Mashariki (EAC) na nchi za kusini (SADC).
Utandawazi ulipamba moto kwa kasi kubwa zaidi katika kipidi hiki cha utawala wa awamu ya tatu.
Athari za mtindo wa biashara huria ya kimataifa zilijitokeza kwa nguvu sana wakati huu. Kushiriki kwa Rais Mkapa katika tume ya kongamano mbalimbali za kimataifa sio tu kuliipatia heshima nchi yetu, lakini pia kuliwafungua macho baadhi ya Watanzania juu ya ushindani mkali wa kibiashara na kiuchumi unaotukabili na nchi zingine.
Haya Mambo matatu hayakuwa mapya kabisa. Yote yalikuwapo siku zilizopita kwa kiwango Fulani, lakini yalipata nguvu sana kuitekelezaji katika muongo huo.
Athari iliyojitokeza zaidi kwa maisha ya Tanzania, Juu ya mambo haya matatu, ilikuwa ni kiuchumi. Serikali za awamu zilizopita kwa vipindi mbalimbali zlijaribu kubuni na kutekeleza mbinu za kusaidia.
Pamoja na juhudi za serikali zetu zilizopita, wabia wetu wa kimataifa nao walitoa fursa mbalimbali ambazo zilikusudia kutuwezesha kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Mifano michache itafaa kuiangalia :-
“Open General License” – OGL ( Tangu awamu ya Kwanza)
“Commodity Import Support” CIS
“Debt Conversion Programme”
“Microfinance Policy”
“Economic Empowerment Policy”
“MKUKUTA, MKURABITA, AGOA, EBA N.K”
Sambamba na hayo, awamu ya tatu ya Rais Mkapa ilijitahidi sana kujenga misingi imara ya uchumi wa Jumla (Macro-economy). Baada ya kuimarishwa utaratibu na tabia ya kulipia madeni, kuongeza ukusanyaji wa kodi, kudhibiti mfumuko wa bei na thamani ya sarafu ya Taifa, kuboresha miundo mbinu ya usafiri na mawasiliano, na baada ya kuonyesha dhamira ya kuipa nguvu sekta binafsi na kuitambua kama mtambo wa kuzalisha mali na kukuza pato la Taifa, wawekezaji walivutiwa na kuanza kuwekeza katika sekta mbali mbali za uchumi.
Serikali ya awamu ya tatu ilifanya marekebisho makubwa katika sekta ya fedha na kuvutia mabenki ya nje kuingia nchini. Huduma za aina hii zilisisimua kwa kiasi kikubwa biashara ya kimataifa katika sekta hasa za madini, Utalii na uchuuzi wa bidhaa na nje na ndani.
Haya yote ni mazuri na lazima yaendelezwe kama ambavyo Mheshimiwa Ras Kikwete ameahidi kuyaendeleza katika awamu ya nne. Lakini ni vema tutambue kwamba mafanikio haya kwa kiasi kikubwa sana yamewagusa Wananchi wachache waliomo katika sekta rasmi ya uchumi.
Watanzania wengi bado wana hali duni ya kimaisha na hawajaguswa na faida zilizopatikana katika sekta ya uchumi wa kisasa. Rais Kikwete ameahidi juhudi za kuinua hali ya maisha ya Watanzania kwa kuwaingiza kwenye njia kuu za Uchumi wa kisasa.
Tunaamini kwamba, kwa misingi iliyokwishawekwa katika awamu zilizopita, hasa awamu ya tatu kiuchumi na tukizingatia neema za maliasili ambazo tunazo nchini, awamu ya nne imekuja na ari ambayo inaweza kabisa kutimiza matarajio ya wananchi. Lakini uwezekano wa kutimiza matarajio hayo utategemea sana juhudi za tawala katika ngazi za serikali kuu, Tawala za Mikoa, Mamlaka mbalimbali za dola, Taasisi mbalimbali za kiraia (Civil society) na hasa juhudi za wananchi kwa jumla wao.
Tukienda pamoja na kushirikiana na kwa kueleweshana juu ya vita vya kiuchumi inavyoikabili nchi yetu, ni dhahiri Serikali ya awamu ya nne itaweza kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi. Neema za maliasili tunazokusudia hapa ni pamoja na watu wenye fani mbalimbali, na wenye moyo wa uzalendo unaowahurumia Wananchi masikini wanaotafuta riziki zao katika sekta ya uchumi isiyotambulika.
Ili tutambue uzito wa tatizo la maendeleo ya wananchi wa Tanzania, ni vema tuchambue jinsi tulivyo!Katika Wananchi takriban milioni 35, nusu yetu ni wazee wenye umri wa miaka 65 na zaidi, pamoja na watoto na Vijana mpaka umri wa miaka 18. Waliobaki ni wananchi milioni 17.5 wa umri kati ya miaka 18 na 65 ambao ndio nguvu kazi wanaobeba mzigo wa kuwatunza watoto, Vijana na wazee.
Takwimu na taarifa rasmi zilizofikishwa katika kamati ya Fedha na Uchumi ya bunge mwaka jana zilionyesha kwamba wananchi wanaotambulika katika sekta rasmi ya uchumi ni milioni mbili tuu.. Hawa ndio wanaofanya kazi za Kuajiriwa na ujiajiri. Ndio wanaolipa kodi kwa utambulisho rasmi, pamoja na kutumia huduma za kibenki na fursa mbalimbali zilizoandaliwa na dola kwa ajili ya maendeleo ya sekta binafsiWananchi milioni 15.5 wanafanya kazi za kila aina, katika sekta zote za uchumi bila kujulikana na vyombo vya dola. Hii ndiyo sekta kuu ya pili ya uchumi usiojulikana kwanjia sahihi na rasmi.
Wananchi hawa wana rasilimali zao ambazo hazitambuliki na kwa hiyo haziwasaidi katika maendelo ya kisasa. Hawakopesheki, hawalipi kodi na hawawezi kutumia fursa nyingi zilizoandaliwa na serikali kwa ajili ya maendeleo yao. Hata hivyo wanaona jinsi nchi ilivyobadilika sura kwa maana ya majengo mapya, mabarabara, magari, umeme, usafiri na mawasiliano.
Wananchi hawa milioni 15.5 wanatambua faida zinazopatikana katika sekta rasmi. Wachache wanaojaonja anasa za utandawazi kwa matumizi ya simu za mkono, TV, na radio. Lakini wengi wao bado wako mbali sana na faida za uchumiwa kisasa ambazo kama tunavyoona zinawagusa wananchi milioni mbili tuu. Na hata hao milioni mbili, ni wachache miongoni mwao ambao ni wachezaji wa kweli katika shuguli za uchumi wa sekta rasmi.
Katika Kipindi cha mwaka uliopita wa fedha 2004/2004, idadi ya akaunti katika mabenki yote nchini ilikadiriwa kama laki tatu tuu (300,000). Sehemu kubwa sana ya hata wao wananchi milioni mbili waliomo katika sekta rasmi ya uchumi hawapati faida ya huduma za benki. Nao pia hawakopesheki katika mazingira yaliyopo hivi sasa.Suala la mzingi, ambalo ni lazima tulipatie jawabu haraka, ni jinsi tutavyoweza kuvuta nguvu zetu za kitaifa ili nchi yetu ikabiliane na ushindani wa kibiashara na kiuchumi katika mazingira haya ya utandawazi.
Tanzania imo vitani. Ni vita ya kiuchumi inayolazimisha tufungue mipaka yetu, siyo tu kwa jili ya bidhaa za kutoka nje lakini pia kwa ajili ya wafanyakazi na wawekezaji ambao wanavutiwa na fursa nyingi za kujitajirisha zilizomo nchini mwetu.Hii ni hali ambayo haiepukiki na wala si busara kujaribu kujiepusha nayo. Tunachotakiwa kufanya haraka sana ni kuwashitua wananchi wetu, kuwasisimua na kuwaanda kwa vita kali ya kiuchumi. Mahindano yetu na nchi zingine yanatutaka tuzalishe mali katika sekta zetu zote za uchumi zitazoongeza pato la Taifa kwa kasi kubwa zaidi.
Tanzania ina nafasi na fursa ya kufikisha katika masoko ya Dunia bidhaa zinazotakiwa duniani. Tusipozalisha bidhaa hizo sisi wenywe pamoja na kushirikiana na tuwatakao kwa mtindo utaolinda maslahi ya taifa letu hivi sasa, baadaye (na baadaye hii ni miaka kama kumi na tano hivyi) Dunia itatulazimisha tufanye kama Dunia inavyotaka.
Kazi ya kuwatayarisha wananchi kwa mapambano haya ya kiuchumi, na kazi ya kuvuta nguvu zote za Taifa kwa ajili ya vita hii, haiwezi kufanywa na Serikali peke yake, Bunge peke yake, Vyombo vya wafanyabiashara au kundi lolote peke yao.Tunadhani ni bora tuunde chombo kitachowajumuisha watu wa fani mbali mbali, makundi ya kila aina, viongozi wa Taasisi za kisiasa, Kibiashara, kiroho na taaluma, Chombo ambacho kitachambua kwa undani mipango yote na fursa zilizoandaliwa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kujiendeleza.
Kwa mfano, ni watu wachache mno wanaojuwa habari za MKUKUTA, MKURABITA na mifuko mbali mbali yenye malengo ya kuwasaidia wananchi. Chombo hiki kitatafiti taratibu zote na fursa zote zilizowekwa na serikali yetu, na hata Taasisi za kimataifa, ambazo zinakusudia kutuwezesha kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Taarifa sahihi juu ya yote haya itakuwa inatolewa kwa namna ya kuwaelimisha watu ili waweze kuchacharika katika sekta zote za Uchumi.
Tunakusudia kuwashwawishi wananchi wanaharakati wa maendeleo, wajiunge na chombo hichi ambacho madhumuni ya msingi ni kuhimiza maendeleo ya wananci kwa kujenga taratibu sahihi za ushirikiano endelevu baina ya serikali na watu.
Tarehe 18 Machi 2006, Jumamosi saa nne asubuhi tutakutana katika ukumbi wa hoteli ya Royal Palm Movenpick, Dar es salaam.Ni maombi na matumaini yangu kwamba utakubali kujiunga na chombo hiki cha kiraia ambacho azma kuu ni kujenga ushirikiano wa dhati na vyombo vya dola ili kwapamoja tupigane vita vya kuondoa umasikini na kujenga uwezo wa nchi yetu kwa mashindano ya kiuchumi na mataifa mengine.
Kujiunga kwako nacho kutakipatia chombo hiki heshima na kutuwezesha tuaminike na tuwe msaada mkubwa kwa serikali katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo.
Tunamini kwamba, pamoja na wewe, idadi kubwa ya wananchi wasiopungua mia moja watakuwa amejiunga na kulipia ada za uanzilishi wa Taasisi hii.
Rasimu za katiba inandaliwa ili baada ya kukubaliwa na kikao, ambacho kitachagua uongozi, tutachukuwa hatua za usajili na kuanza shuguli zitazokusudiwa.
Sunday, February 19, 2006

Maswali nane yenye hatima ya Tanzania kiuchumi!
Pichani - Raisi Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) wa Tanzania akisalimiana na Gaudensia Temu, katikati ni Bwana Elvis Musiba (Mwenyekiti TPSF)alipokutana nao kwenye maakuli yaliyoandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF).
Wasomaji wapendwa, natumaini ilikuwa ni wiki yenye pilasi pilasi (pilika) nyingi huko na kule ilimradio tu kujitahidi kuwa raia mwema na mwenye wajibu kwa ulimwengu huu maana ni dhambi ikiwa watu wengine watakuhudumia na wewe usijitahidi kuwahudumia pia...haina maana kuwa kwa sababu ulimlipa daktari alipaswa awepo akutibu kwa sababu tu ni wito...inabidi tukumbuke kuwa alipoamua kukaa mbali na mapenzi wakati akisoma kama wazee walivyotuasa, alipoamua kuweka michezo kando, alipoenda chuo kikuu na kufukuzwa mara nane, alipocheleweshewa kialowance, alipokosa usingizi ili asome na kufaulu, alipotakiwa kupasua maiti, .......sisi tulijichanganya kwenye starehe, michezo ikawa dira, walipofukuzwa tuliwaita wenye utovu wa nidhamu, tulianzisha biashara mtaani, tulilala si chini ya masaa 8 ambayo hushauriwa kiafya, na hospitali huenda inapobidi....tofauti ni kuwa sisi tulioanza mapema hatuna shaka sana kwani biashara ndio zimeishachanganya, na watoto ndio hao wanakaribia maliza shule sembuse huyu daktari ambaye tulianza nae la kwanza, kukaachana alipoenda kidato cha kwanza na leo eti anakuja akitaka mchango wa harusi!!!! hivi atafika kweli?
duniani kuna migongano mingi sana ambayo imejengeka katika misingi ya siasa uchumi na yote hiyo ni kuleta maendeleo. hivi majuzi wenzetu (wanaoona mbali???) wameongeza neno umasikini katika defenition ya Uhuru...kuwa huwezi kuwa masikini ukajiita uko huru ....hili nakubaliana nalo!!hii inamana nchi karibu zote za Afrika si huru!!
ubepari umejengwa katika dhana ya kutumia mazingira yaliyopo kwa manufaa ya jamii - wahusika. ni kweli wakati wanatuletea sera za kuhifadhi mazingira wao sijui kama wanahifadhi kweli? nimesikia huko ulaya wenye viwanda ili wapewe vibali vya kufanya kazi imebidi wawe na eka kadhaa za misitu popote pale ulimwenguni na ikibidi Afrika kunyonya uchafu wanaoupuliza hewani! mahesabu ya uwezo wa kunyonya uchafu hufanywa kushirikiana na Taasisi zetu za utafiti...siku hizi pia wanatumia remote sensing...wanaangalia toka juu kwenye satelittee hawahitaji sana kuwasiliana na sie! wanangalia Leaf Area kama ina uwezo wa kunyonya carbon dioxide...ndicho tu wanahitaji...sana sana watatumia watunga sheria wa nchi husika na taasisi zake kuhakikisha misitu inatunzwa...watatoa land cruiser moja na mishahara ya kulipa watafiti kwa mwaka ....yaani watafadhili!!
wote tunakumbuka jinsi Joji Kichaka (George Bush kwa mujibu wa Ndesanjo nadhani ni mwaka juzi alitoa ruhusa kuvamia milima ya ??? (nimesahau jina - mtanikumbusha hapo) kuchimba makaa ya mawe. alifanya hivyo akijua wazi anaharibu misitu iliyokuwa ya hifadhi...lengo lake lilikuwa ni kutoa ajira kwa raia wake ambao walikuwa wanaandamana kila siku kutaka ajira....nadhani ilibidi kuwa na kipaumbele! ajira zikaishinda uhifadhi maliasili...hata hivyo hakuna haja ya kuogopa kwani kuna misitu mingi afrika!! wote tunakumbuka jinsi Joji Kichaka alivyovuruga uungaji mkono wa Kyoto protocal ulioanzishwa na raisi aliyetangulia Clinton..... alikataa kuunga mkono mkataba huo akisema "the energy demands of the United States are Un negotiable" - ulimwengu ukagwaya, lakini wote tunakumbuka jinsi Joji alivyopata madaraka - aliungwa mkono na CIA na watu wanaojua jinsi ya kurekebisha mambo kwa manufaa ya taifa, waliona kabisa kuwa Clinton alikuwa anawapeleka kusiko....wote mtamkumbuka jinsi Joji Kichaka alivyokashifiu sera za Clinton kuwa anazunguka duniani kuhubiri amani!!! amani ya baba yake wakati watu wametengeneza cluster bombs na zikawa zinaozea ndani? hiyo mikopo iliyotolewa na benki nani angerudisha?? hapo nikamuunga mkono jamaa yangu Professor Toongolay (kutoka Zimbabwe - sio Sri lanka) kuwa Afrika itakaa sawa pale tu kutakapokuwa na Taasisi zisizofuata upepo wa kisiasa! rejea jinsi taasisi za marekani zilipoamua kuwa Kichaka atawafaa zaidi ya Gore!
wote tunajua duniani kote kuna mgogoro! mgogoro wa nishati! kumbuka mzozo wa Korea Kaskazini na Marekani! Marekani waliahidi kuisambazia nishati kwa njia ya mafuta Korea Kaskazini ili iachane na mpango wa kuzalisha nishati hiyo! hivyo kufanya eneo lile lililokuwa na mzozo wa kivita (korea kaskazini na Kusini) kwa ajili ya umashariki na umagharibi ......Marekani hawakuwa na nia njema kwa Korea Kaskazini kwani walianza kuwatosa Wakorea Kaskazini kwa kuacha kuwapelekea nishati...walisema kwani sisi baba yao? - Korea kaskazini wakijua umuhimu wa nishati kwao, wakarudia mpango wao wa nishati ya nuclear!
Leo hii tunaona Iran nao wanaitwa kuwa ni magaidi kwani tu wameliona hilo la nishati kuwa ni la msingi na wameanza kampango kao ka kutengeneza nishati!! serekali ya Iran imejitahidi sana kuuelimisha umma wa dunia kuwa kazi yao haina chembe cha ugaidi, na ni kwa ajili ya nishati tu! tunaona jinsi kiongozi wa Iran anavyojitahidi kupeleka matabu yake kwa Mohamed Baradou (mkuu wa shirika la UN la kudhibiti mionzi) lakini Marekani hawataki kuelewa somo....wakisisitiza azma yao ya kuitwanga Iran. Iran nayo imekuwa ikiomba umoja toka kwa nchi zinazoendelea ikiwepo nyingi za Afrika...nakumbuka juzi wakati Marekani ikiishutumu Iran, Kiongozi wa Iran alikuwa hapa SA akijaribu kutafuta uungwaji mkono!
Utandawazi uwepo, haki nayo pia ni msingi iwepo! je hawa wenzetu wa magharibi wanaogopa nini kwa sisi kuwa na nishati za namna hizo? labda wanajua tutatoa ushindani halisi katika utandawazi? maana wao wenzetu wanafanya kazi usiku na mchana hivyo wakati sie tunamaliza mwaka, wenzetu wamemaliza miaka miwili. Kakobe alimpa changamoto JK kuhakikisha kuwa watu wapige mzigo masaa 24!! nadhani wanajua pia kuwa teke linalokujia ndio njia pekee ya kujenga misingi imara ya unyonyaji - hapa labda tufananishe kuuza gunia moja la mahindi ili kununua air time ya dola kumi ambayo pia inaexpire mwisho wa mwezi!!! - basi kuna haja gani ya sisi kuendelea kulima mahindi au kahawa ambayo kila siku inashuka bei kwenye soko la dunia? kwa nini na sie tusifikirie kuanza kutengeneza kompyuta badala ya mabadilishano haya??
ninrudi kwenye hili la rasilimali. niliwahi kusema kuna shule mbili za rasilimali. ya kwanza inaamini kuwa kuna siku rasilimali/madini yataisha (ikiwepo mchanga) na hivyo dunia kuishiwa. kwa namna hii shule hii huamini kuwa madini yanapopotea basi yale machache hupanda bei!! Shule ya pili huamini kuwa kwa kutambua kuwa binadamu ni mambo zooose (ultimatum resourse) - mwisho wa dini / rasilimali moja ni mwanzo wa lingine!
Katika hizi shule mbili ninaliona hili la pili ni la ukweli zaidi. kwani nani alijua kuwa tunaweza kuacha kutumia mbao kutengeneza fanicha? nani aliwahi kudhani kuwa unaweza kuwa na viatu vimetengenezwa kwa plastic na sio ngozi? nani aliweza kujua kuwa dhahabu itashuka chati na risasi kupanda chati? nani alijua nani alijua? wote tunajua kabisa kuwa teyari wenye makampuni ya magari wameishatengeneza magari ya solar. ya umeme teyari hata pikipiki nimeziona hapa afrika kusini! je tunakumbuka wakati Kichaka akijiandaa kumtwanga Sadam alipata upinzani toka kwa Ujerumani na Ulaya? je tunakumbuka jinsi mara pale pale Joji Kichaka akatenga mabilioni ya dola kufanya utafiti wa hydrogen car? alijua kabisa kuwa waarabu wanataka kushikamana na wazungu wa ulaya hivyo akawa anawatafutia dawa kwa kuua mtaji wa mafuta yao!!
kwa kuwa sijapata muda lakini kwa miaka takriban miwili nikiwa hapa Afrika Kusini nimekuwa nilifuatilia jinsi uchumi wao unavyozunguka....dola hupanda chati nadhani kuanzia kati ya mwaka hadi pale mwanzoni huanza kushushwa tena....kwa mzunguko huo huo ....utakuta thamani ya dola kwa rand inacheza kati ya 1:5.99
hadi 1:6.7.....haingooki zaidi ya hapo. juhudi za kutunza rand yenye nguvu hufanywa na serekali na gavana wa bank kuu!! wanachofanya ni kuongeza uzalishaji kutumia rasilimali zao ili kukabiliana na mawimbi...hakuna asiyejua nadasi ya madini mfano mafuta na dhahabu sijui gavana wa Tanzania hufanya nini zaidi ya kutia saini kwenye noti!!! huyu gavana Tito Mboweni ana nguvu pengine kuliko hata raisi...labda na ndio maana husemwa Gavana ana mshahara mkubwa kuliko raisi......ndio husema kuwa nchi inahitaji wataalamu wa kukodi ikibidi tanzania, huongelea kilaaaaa kituuuuuu!!! huongelea masoko ya ajira, huongelea uzalishaji, akiba kila kitu! !! kuna namna wanacheza na maliasili zao kupambana na mifumuko...huongeza uzalishaji wa madini yao kama vile mafuta na madini mengine..... na kila kitu kupambana na mfumuko......hivyo maisha kuendelea kuwa murwa kwa wananchi wake na uchumi wake! wanachimba mafuta na pia wana mitambo ya nishati ya nuclear! kong'oli hapa- ninavyoandika makala hii kesho wenyeji wa Western Cape wameandaa maandamano kupinga kukatiwa umeme kutokana na matengenezo wa plant ya umeme!!
turudi kwa Tanzania yetu! tuna kila kitu cha kufanya watu waishi vizuri, pavutie kuwekeza, na kupambana na mifumuko ya bei, kutoa ajira n.k. kila kitu ni swafiiiiii!!! sio siri iko wazi kuwa hata wengi wetu nyumba zetu zimejengwa juu ya migodi, nilisikia pale mt uluguru pia kuna uranium ya kutosha(uranium ni madini ya kinuclear ambayo yanatumika kutengenezea nishati - nchi nyingi huagiza madini haya ili kutengenezea nishati . hutoa nguvu yanapomwagiwa maji kwenye planter na kufumuka na nguvu inayofanya umeme usikosekane nchi za wenzetu)!! ni nini basi kinatufanya nasi tusijitahidi kuwa taifa la kisasa? lenye kutumia maliasili na rasilimali zake kunyanyua hali za maisha za wananchi wake? tunasubiri yaishe kwa wenzetu ili tuanze kuuza kwa bei kubwa? manadhani hiyo itatokea? nani alijua kuwa leo hii dhahabu itakuwa haina dili?? tuna uhakika kuwa yale mafuta yaliyopo Tanzania yatakuwa na msaada ikiwa hydrogen car itaingia mtaani?? je sasa na vijana tunaoshindwa kuwapeleka shule kwani nchi haina uwezo wanaweza kufanya lolote tukianza chimba mafuta yetu?? - mimi msimamo ni pambana na matatizo sasa hivi, yatabebesha neema kwa kizazi kijacho!! - naamini katika shule ya pili ya wanarasilimali asili...
kwa namna hiyo hiyo, juzi mheshimiwa kiongozi wetu mkuu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alitoa hotuba moja yenye mguso sana.....ilivyoonyesha kuwa yeye kamna mwanasiasa anahitaji nini kutoka kwa sekta binafsi...na hivyo kuonyesha umuhimu ushirikiano na sekta binafsi kuboresha maisha ya watanzania wote! - aliomba wasisite kumfahamisha mahala rushwa inapokwamisha mambo ili aikarabati once and for all!!! - hala hala lakini kumbe hata na yeye amekuwa akilala usiku kucha kuwaza tatizo la Tanzania ni nini hasa inapokuja kwenye matumizi ya maliasili? hotuba ya Kikwete
ninatumaini wote tulikuwa pale kwa bwana Mwaipopo tukaona jinsi kikaratasi chake kilichodai maji ya nile ambavyo kikatupiwa kapuni, licha ya afrika kuitwa nchi moja ilhali Luxembourg ambayo imezidiwa ukubwa na baadhi ya mikoa yetu ya Tanzania ikaitwa kwa majina! tunaona jinsi kiongozi wa Ethiopia anavyoyalaumu mashirika haya haya ya UN yanavyomkatili kumsaidia akiomba miradi ya umwagiliaji
Nile ni ya nani?
Pamoja na kuwaomba wote kuisoma hotuba inayotia uchungu ya raisi pia tusaidiane jinsi ya kuyajibu........ninakumbusha kuwa kuandika habari hii ni moja ya mchakato wa kuijenga Tanzania ya ndotoni Jeff Msangi Maswali ambayo mheshimiwa raisi Jakaya Kikwete aliyauliza ni haya yafuatayo!!!
Allow me to leave with you some few questions to ponder as you prepare for the first TNBC meeting and IRT meetings. I am doing this to stimulate a healthy discussion during those meetings hoping that at the end of such a discussion, you will come up with solutions to the challenges:
1. Tanzania is renowned for abundance of natural resources - such as arable land, mineral deposits, and natural attractions - that are mostly under-utilised. There are also opportunities in infrastructure, utilities, transit trade, and aviation. It is a fact that very few African countries can claim to supersede Tanzania on this score. However, we need a fresh look at what is it that impedes speedy exploitation of these resources and opportunities to the benefit of the country. We know that full utilisation of these resources would enable Tanzania achieve higher growth rate which we need badly for eradicating income poverty and overcome underdevelopment? What can business do to deliver on this front tangibly and in a sustained manner?
2. Few countries in Africa can claim to enjoy the kind of political stability that Tanzania has. The issue at hand is how can we, together, make use of our political stability as a resource and foundation for growth and poverty eradication?
3. The benefits of the correct economic and fiscal policies that have been applauded by many are yet to reach the ordinary Tanzanian. We have in place the right macro-economic fundamentals for promoting growth, investments and trade. The challenge before us is how to speedily and consistently send the gains to the micro-economic level and to rural Tanzania. Failure to do that, the macroeconomic gains will remain meaningless and illusive to the majority of Tanzanians. How do we, together, you and us, ensure that gains reach the micro-economic level?
4. Tanzania is widely acknowledged as having one of the most favourable investment incentives regimes worldwide. Transfer of capital and profits is allowed, and currency is freely convertible. Repatriation of profits, dividends, royalties, and such other payments are freely allowed. Investments are protected against arbitrary nationalisation and expropriation. A commercial court has been established, and international arbitration is provided for. Inspite of all these achievements, we are yet to witness a commensurate flow of investments. Can we know why? And, more importantly, what else needs to be done for us to witness an investment flow deserving a country like ours? Can you also suggest a regime of incentives to revolutionise the agricultural sector and ensure empowerment.
5. While the Tanzania Investment Centre has now been strengthened to be a truly one-stop centre, assisting investors in all issues, are we confident that ample assistance is given to locals and in establishment of indigenous enterprises? What can Corporates contribute in this front?
6. The other important matter that is more or less related to the previous one is that of creating a sizeable Tanzania middle class. Is it there? Not really! You will agree with me that the existence of a large middle class is critical for business and growth. How do we create it? What can the corporate sector and government do? We have to have answers to this pertinent question.
7. Tanzania qualifies for preferential trade access to the European market, under the EBA - “Everything But Arms” - arrangement provided unilaterally by EU to ACP countries. Tanzania has access to similar facilities for the US market, through AGOA, as well as Japan, China and Canada through more or less similar arrangements. So far, we have not utilised these facilities as some of our neighbours have been. The questions are why not and what do we do? We need to have answers quickly because these are very important facilities in propelling faster economic growth and development. Besides, these facilities are not there forever, they have a limited life span. We better utilise these opportunities before doors close. How do we catch up?
8. Finally, Tanzania is well-positioned geographically. It is a gateway to six neighbouring countries, five of whom are landlocked. Tanzania enjoys a larger market within the regional economic groupings to which we belong - the East African Community and the Southern African Development Community – which together provide a market of almost 250 million people. Given this enviable position, the challenge and the question is how is the Tanzanian Private Sector poised to take advantage of this niche and exploit the geographical location to turn Tanzania to a lead economy within the region? And, what is it that is needed in order for you and us to rise to the challenge in a sustained manner? As businesses, have you really positioned yourselves well enough to take advantage of the EAC and SADC common markets? If not, why? Let’s put our act together to benefit from these lofty opportunities.
namtakieni nyote mwisho mwema wa wiki!
alamsiki!
Saturday, February 11, 2006
UKISHINDWA KUWAJIBIKA MSINGIZIE ANAYEKUHOJI KUWA NI MPINZANI, UMEMALIZA MCHEZO - IZE !!!- TENA RAHISI SAAANA !
Katika hotuba ya Rais Kikwete hivi karibuni alisema wanaoshindwa kuwajibika wakiulizwa wanaweza kuja kusema wanaowahoji ni wapinzani kumbe ¨sio ni kada wa CCM. - KIINI CHA MJADALA!
Asalamu alykum wanablogu wote popote pale mlipo ndani au nje ya Tanzania. basi ni kajioni haka ka leo mzee mzima nishajisweka ndani ya msuli taratibu nakodolea macho tarakilishi yangu nione kama ninaweza kuchangamsha safu japo kwa mwisho huu wa wiki. Tanzania ya kikwete naifurahia sana kwani kuna kila dalili kuwa tumepata kiongozi mkuu (Jeff alituomba inapobidi tusifie - www.harakati.blogspot.com) ambaye huongoza na kutangulia kwenye kero wakati wengine wakifuata. hii imesifiwa kuwa ni njia njema ya kuwawajibisha walio chini. juzi nikiuwa ninasoma kupitia wenzetu http://www.uchaguzitanzania.com/new/articles/4048/1/Kikwete-atoa-mpya,aibukia-masoko-ya-uswahilini kuwa utaratibu wa kutembelea masoko na maeneo husika umewafanya viongozi kuwa makini saa zote kwani hawajui siku wala saa..na mara nyingi wamewasiliana kwa viselula kuwa anakuja mchana ...utaratibu huu teyari umeishaanza kujibu kwa kazi kuonekana na kero kutafutwa..rejea habari ya pasipoti..hii imenfanya hata mkuu wa the Full Gospel Bibke Fellowship Askofu Kakobe miongoni mwa watanzania wengine kummiminia sifa...
http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/02/11/59876.html penye kusifia na tusifie. hongera Askofu Kakobe
kwa namna hiyo hiyo wakati akiapisha wakuu wa mikoa wapya aliwaomba wafuate namna yake ya utendaji kazi (kwa kutokukaa ofisi kuachia watendaji wa chini wafanye kazi)..http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2006/02/11/59822.html
pia wakati huo huo amelaumu jinsi ushikwaji wa pesa za halmashauri umekuwa mbovu (rejea hizi kulipia madeni na hizi kulipia madeni mengine kwenye makala iliyoitangulia hii). nadhani kwa mwendo huu tunaweza kufikiria mara mbili hisia zetu kuwa serekali za majimbo zitakuwa na majibu ya matatizo yetu zaidi ya ilivyo sasa. pia itasaidia kutowaona wakuu wa mikoa na wilaya mizigo. tunawaomba basi wakuu wa wilaya na mikoa wajishughulishe zaidi na kutekeleza ilani zilizomweka raisi wao madarakani badala ya kujipigia kampeni binafsi au za vyama na kukandamiza mawazo hai. kampeni ni kutekeleza sera kwa faida ya maendeleo ya umma.
wiki hii nzima ilopita kumekuwa na mjadala motomoto kuhusu wimbi jipya la ujambazi kutisha. wimbi la ujambazi lilimfanya JK aunde wizara malumu ya kushughulika nao. na kutokana na uzito wa suala hilo, ilibidi iwe ni wizara ya mwanzo mwanzo katika mpango wake wa kuzungukia wizara. Kama kawaida yake Raisi JK hakuanza kufakamia vibanzi vilivyopo kwenye macho ya wenzie BALI ALIANZIA KWAKE akisisitiza kuwa kuna haja ya jeshi hilo kujisafisha kwani wapiga kura wamekuwa wakilalamika kuwa limekuwa likiwauza katika juhudi za kukabili ujambazi. http://allafrica.com/stories/200601230271.html Mheshimiwa JK alifuatiliwa na waziri wake Mh. Bakari Mwapachu aliyelitaka pia jeshi hilo lijisafishe http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2006/02/03/59223.html
Jeshi la polisi tanzania kwa karibu muongo mmoja linaongozwa na Ndugu Inspekta Jenerali Omari Iddi Mahita ambaye CV yake niliifuma mahali http://www.theiacp.org/div_sec_com/div/MahitaBio.pdf japo siwezi kuhakikisha kuwa iko sahihi au la. lakini hata hivyo tunaweza kukipima cheti kwa jinsi mtu anavyotenda au kuongea nawaachia hilo wasomaji.
kwa wafuatiliaji wa mambo ya ndani ya nchi ni kweli kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu jeshi hilo na kufikia kipindi watu wakasema kuwa kuna haja ya jeshi hilo kuundwa rasmi, na ikibidi kiatu cha kigogo wake kivaliwe na mwanajeshi kutoka nje ya jeshi hilo na labda JWTZ kwani ndiye atakayeweza kusafisha uozo ndani yake http://www.uchaguzitanzania.com/new/articles/4046/1/IGP-ateuliwe-kutoka-JWTZ ...yote hii ni kutafuta suluhisho la tatizo....
pia habari kutoka ndani ya jeshi hilo zinaonyesha kuwa hata askari wadogo wamechoka na kuamua kukiri ukweli kuwa wanakwamishwa kazi kutoka maafisa wa juu. wanadai wakishika wahalifu wanaishia kunyanyaswa, na mara nyingine hupewa lita kumi kufanya patrol siku nzima. kwa namna hiyo na mambo mengine mengi walimuandikia waziri wa mambo ya ndani wakimsihi kuwa wanalo tatizo la jeshi na kuomba kuonana naye bila kuwepo uongozi wa juu wa jeshi hilo...yote ni kutafuta suluhisho la tatizo.......
wabunge wa bunge letu tukufu pia waliweka bayana kuwa kuna tatizo ndani ya jeshi, ambapo walitupa lawama za moja kwa moja kwa mkuu wa jeshi la polisi kuwa hafanyi kazi zake kama polisi bali mwanasiasa mkereketwa, na hivyo kutoka nje ya maadili ya kiutendaji. walimuomba ajifunze kufanya kazi kama wakuu wengine waliokuwapo kabla yake wakati wa Nyerere....yote ni kutafuta suluhisho la tatizo.......maoni ya wananchi, hoja za wabunge na kilio cha polisi wa chini vilipelekea karata ya kibarua cha Mahita kuwa mkononi mwa raisi JK http://www.ipp.co.tz/ipp/alasiri/2006/02/08/59642.html ......yote ni kutaka kutafuta suluhisho la tatizo...........
Mkuu wa polisi naye bila simile akirudia kusa la kukabiliana uso kwa uso na wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa mara ya pili (mara ya kwanza alihusisha utendaji mbovu wa jeshi na mishahara midogo - ikabidi aangukie). kwa kweli kwa mtu wa kawaida ni kitu cha kushangaza kuwa aling'aa kwenye ukurasa wa juu wa http://www.skyfm.co.tz/ipp/nipashe/2006/02/10/59752.html ameshika MAJIBIVISU YA KUTISHA YENYE RANGI NYEKUNDU...habari hiyo pia ipo hapa http://www.uchaguzitanzania.com/new/articles/4091/1/Singatuki-Mahita kuwa kuandaa ujambazi imekuwa ni kazi ya CUF wakimalizia hasira za kushindwa uchaguzi kwake. alikiru kuwa amekuwa ni mwiba katika kasi ya kwenda ikulu na atahakikisha kuwa CUF hawaingii ikulu.....labda kabla ya kuendelea tuujadili umungu mtu alionao huyu bwana na labda pia uwezo wake kwa nafasi alionao(graduate wa ontario police college - Canada - rejea CV)halafu tuendelee.
1. hii ni mara ya pili Mahita kutukana wabunge - mara ya kwanza aliwaangukia wakamsamehe
2. Mahita anaonekana hajui mipaka ya kazi yake (kashindwa kutofautisha mbunge ndani ya bunge na nafasi yake katika uongozi wa chama)..mbunge ndani ya bunge yuko haijali ni CUF au CCM ni juu ya Mahita kisheria na si vinginevyo.
3. kashindwa kutofautisha wakati wa kampeni na wakati wa kazi kwa mbunge
4. kajitaja wazi kuwa alihakikisha kuwa CUF haishindi na ataendelea na msimamo huo
5. ni aina ya viongozi wasiotakiwa sasa..miaka mingi tulizoea kuona viongozi wabovu wanabebwa kwa kujigundisha na CCM...wakidai kuwa wale wanaotufaa ni wapinzani, wana ukabila n.k. amesahau kuwa hata CCM ya wanamtandao imepania kusafisha makunyanzi.. Katika hotuba ya Rais Kikwete hivi karibuni alisema wanaoshindwa kuwajibika wakiulizwa wanaweza kuja kusema wanaowahoji ni wapinzani kumbe ¨sio ni kada wa CCM.
6. anaikumbusha CCM kuwa wakati umewadia kulipwa fidia..ina maana anamtishia JK kuwa bila yeye hakukuwa na kitu ?????? ni kweli????(mtihani)
7. amekataa kukiri udhaifu wake uliomwagwa bungeni (kuchanganya siasa na upolisi) na sasa hivi kajikita kwenye siasa rasmi.
8. kawahakikishia watanzania yeye ni IGP wao hadi kustaafu watake wasitake (mungu kamuhakikishia)
9. kawatishia maisha watanzania wanaolikosoa jeshi (majina anayo).....
10. amekaidi kauli ya waziri wake kuwa jeshi linatakiwa kujisafisha....pia kamuaibisha/ kapingana na raisi wake kuwa kuna tatizo ndani ya jeshi....
12. amedai kuwa CUF inataka kuleta machafuko kwa kumtaka astaafu...hii ni hatari sana, wakati watu wanavunja mgawanyiko wa uchaguzi wakitaka JK afanye mpango kumrudisha mrema kwenye kitengo yeye anavunja zaidi....
13. amefananisha dhamana aliyopewa na umma wa watanzania wote (bila kuhoji chama) kuwa sana na mchezo wa kupokezana kijiti....na ikifika muda wake basi mngine atapokea - amedhalilisha umuhimu wa dhamana yake rejea kwa www.issamichuzi.blogspot.com aliitwa mtu muhimu. ina maana ufanisi kwake sio jambo la msingi bali ni ajira kama nyengine!
14. alisema alizaliwa siku moja na siku moja atakufa..hivyo hana wasiwasi wowote.
kwa kweli umma wa watanzania umeshtushwa sana na kauli ya muheshimiwa waziri mtarajiwa (akiishaupata ubunge)..http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/02/11/59834.html wakishangaa kuwa kumbe alikuwa anawajua majambazi halafu anakaa kimya....na wakati huo huo hivyo kuufanya urejee maneno ya mheshimiwa raisi.....badhi ya kumbi za mijadala zinasema ifuatavyo http://www.darhotwire.com/dar/maoni/15517.html
wananchi na vyama vya siasa navyo vikijianda kumkarabati
http://ippmedia.com/ipp/guardian/2006/02/11/59821.html
http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/02/11/59847.html
cha ajabu waziri wa usalama alititoa kumtetea japo si kwa nguvu kuwa yu safi, labda ndio tofauti ya wanasiasa na waropokaji kama sie!!
http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/02/11/59877.html
siku moja tu baada ya kauli ya IGP tunasikia habari kuwa polisi wamekabiliana na majambazi waliojikita pemba
http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2006/02/11/59819.html
hii inanifanya sasa kuwa na wasiwasi na jeshi hili ukizingatia hata yale matukio ya milipuko miaka ya nyuma ambapo Mkuu huyu amekuwa anawarukia tu CUF ambao nao husema watamshtaki
http://ipp.co.tz/ipp/nipashe/2004/04/07/8460.html
mwalimu wangu wa historia kidato cha kwanza alinifundisha kuwa historia hutufundisha yaliyopita ili tuweze kuganga yajayo. sasa hivi kutokana na tukio hili la utendaji wa polisi (kuua raia wema wakisingizia kufanya kazi, wakidai walitupiana risasi ilhali inadaiwa sio hivyo, na jinsi lawama za siku za nyuma kwa chama cha CUF toka kwa IGP, kushindwa kudhibitisha kuwa CUF wanahusika na milipuko, na hizi mambo za sasa)... bungeni kuna kila haja ya kuamini kuwa mchawi wa Tanzania yenye demokrasia changa ni huyu mhitimu wa chuo cha polisi Ontario!!!
inawezekana matukio yote ya kutia vinyesi kwenye visima, milipuko ya visiwani, majibivisu aliyoyakumbatia, yalipandikizwa na hivyo kuwa propaganda dhidi ya CUF. kuna haja kamili ya kuamini hivyo kwani mbona hatuoni Lipumba au Hamad washtakiwe kwa makosa hayo? mbona tunaona visu na hatuoni majina ya watu waliokamatwa nayo??
1. amekuwa ni mtu wa kwanza kuhakikisha kauli iliyozoeleka kutafuta kimbilio la kutowajibika kuwa wale ni wapinzani.....wale wapinzani wale wakabila wale maadui wa muungano...... wapo wengi tu....huu ni mwanzo tu...... JK hakukosea.......
2. anataka kulitumbukiza taifa katika janga kuu kwa kutowajibika kwake
3. role conflict, ameshindwa kukiri kuwa umma ndio mwajiri wake na amesisitiza kuwa vigogo wanamuunga mkono..... amesahau UGOGO hautokei juu bali ni maamuzi ya umma..... amesahau kuwa bosi wake - mkuu wa nchi yuko ofisini kwa ridhaa ya 80 % ya wapiga kura na sio yeye binafsi!
4. ni mharibifu wa demokrasia changa pia amani na utulivu wa taifa letu. anadiriki kupeleka askari kupiga kura visiwani, na kuadhibu wannchi wanaohoji uhalali wa kupiga kura.....ngunguri...sijui aliombwa au alijipendekeza??????? matukio mengi yanayoonekana yanapitia kwenye vyombo malimbali (bahati mbaya vya si vya nyumbani)...CUF wao wameendelea kuonyesha msimamo wao wa amani na mapatano http://www.cuftz.com/news/ siku chache zilizopita kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed alizitaja sababu tatu zinazodidimiza demokrasia Tanzania kuwa ni VYOMBO VYA HABARI, TUME ZA UCHAGUZI na VYOMBO VYA DOLA akitolea mfano vyombo vya ulinzi "http://www.uchaguzitanzania.com/new/articles/4069/1/Lowassa-atoa-miezi-mitatu-waliofaulu-la-saba-wasome/print/4069.
5. anaharibu pia misingi ya utaifa wetu. kitendo cha kuua raia wengi wa pemba, na kuvuruga chaguzi na amani za wenyeji wa tanzania na hasa visiwani, ndio vimepelekea kwa kiasi kikubwa wananchi kuanza kuhoji juu ya uhalali wa muungano!!!!! kwani umekuwa hauwatendei haki - ukifuatilia historia kilio cha ndugu zetu wa visiwani kwa kiasi kikubwa kimechochewa na mhitimu huyu wa chuo cha polisi Ontario...hivyo kuchochea UFA katika taifa. http://www.ippmedia.com/ipp/observer/2006/01/01/56956.htmlhttp://www.unpo.org/news_detail.php?arg=58&par=3672
...sipingi madai haya na wanachosema, ila juhudi za kuziba ufa zisivurugwe kwa makusudi....au kwa kuleana "u-mwenzetu syndrome" - rejea barua kwa raisi mpya wa Jamhuri.
6. lakini wanasema mwana humranda babaye. wote tunakumbuka jinsi serekali ya Bw.BWM ilivokuwa haitaki kusikia kitu kinachoitwa kukosolewa na hivyo kulea uzembe miongoni mwa watendaji serekalini na kukuza rushwa. bwana Omari kama mtoto basi anafanya alivyoelekezwa na babaye BWM! - kumbuka marufuku ya HAKIELIMU.
ndugu wanablogu na watanzania wenzangu...hiki ndio kilio changu cha kila mara!! je FAHARI UMOJA AMANI NA UTULIVU WETU KAMA WATANZANIA IPOTEE KWA AJILI YA MASLAHI YA MTU MMOJA au kwa ajili ya U - MWENZETU SYNDROMME?
tatizo ni kuwa siku zote matatizo yataishia kwa wananchi masikini ambao ni wengi na wa kawaida ambao riziki zao ziko pale wanapokanyaga na hawawezi kujilipia chakula sembuse ulinzi....viongozi wao huendelea kuwa salama na hujilinda http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/01/12/57640.html
alamsiki!
Saturday, February 04, 2006
tunahitaji kuwa wazi na wenye nia moja!
subhakleri waungwana. ni majuzi tu nilikuwa jamvini kwa bwana mwandani nikwa ninajaribu kumshawishi kuwa kuna haja kubwa kushughulikia vibanzi ndani ya macho yetu kabla ya kuanza kushambulia ya wenzetu. nia ya usemi huu ilikuwa ni kuwa sehemu kubwa ya matatizo yetu tunayasababisha sisi wenyewe. ...
Mpendwa raisi wetu Mh. JK juzi alikuwa kwenye safari zake za kawaida kutembelea mawizara. akiwa pale TRA alisisitiza umuhimu wa TRA kujibidiisha kukusanya kodi na kuziba mianya. Ukweli unabakia kuwa hata hivyo, haitajali kuwa ni kiasi gani cha mapato ya taifa yatakusanywa ikiwa pia upotezaji na matumizi mabaya ya fedha hizo hayatadhibitiwa. leo hii nikisoma http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2006/02/04/59284.html tunaona jinsi ambavyo sekta hii ya habari ikihusu both print and electronic media ikisisitizwa kusaidia vita dhidi ya mdudu rushwa na zoezi zima la usafishaji wa serekali....tunashukuru kuwa sasa waandishi mawepata meno (Baraka kutoka juu). tunaomba mungu zoezi liende vyema. pia labda kina ndesanjo mtasaidia hapo...nadhani hata sisi tunahusika kupitia jimbo la wahariri / waandishi wa electronic media..........kama ni hivyo basi, kwa kifupi raisi anahitaji msaada wetu! kwani Ulimwengu amekiri kuwa kipindi cha mbabe Ben rushwa na ten percent zilipaliliwa na kulindwa kwa nguvu zote, http://www.darhotwire.com/dar/Habari/2006/02/04/15181.html wachilia mbali kutotaka kuelezwa madhaifu ya serekali e.g. Mungai na HAKIELIMU.
ni kweli mafanikio makubwa yapo kupitia maoni yetu. ni juzi tu passport zilikuwa ni kero, leo hii nasikia wanapiga simu kukuita kuwa pasipoti yako i tayari? http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/02/04/59334.html IPP na DHW waliendesha utafiti ambao uliibua kero hii!! wachilia mbali vilio vyetu kuhusu vifo vya mazingira ya biashara na mashirika yetu http://www.uchaguzitanzania.com/new/articles/3998/1/Aiagiza-TRA-kuzidisha-kasi-ya-ukusanyaji-kodi
sasa basi sina nia ya kufanya risala bali ni kuibua kimbembe cha matumizi ya fedha za serekali. Ni majuzi tu tulipata habari ya kusikitisha toka kule Shinyanga ambapo milioni 700 za watoto wa shule zilipotea bila maelezo kumsababisha Waziri mkuu kutaka maelezohttp://www.uchaguzitanzania.com/new/articles/3980/1/Lowassa-atoa-siku-21-kupewa-maelezo-ya-sh.-milioni-700-Shinyanga ...kwa kweli ambao ulitolewa hata sisi ambao sio wahasibu kitaaluma tunashanga ufafanuzi utaona eti kulikuwa na kulipa madeni kwa kifupi mchanganuo ni; Sh. milioni 24. 9 zilitumika kulipa madeni ya NSSF, Sh milioni 73.8 kulipa madeni mbalimbali ambayo hakuyataja. Sh. milioni 54.7 zilitumika kuwalipa wadai washauri, Sh. milioni 8.7 walilipa kama viiunua mgongo, sh. 47.9 zilitumika kulipia saa za kazi za ziada na sh. milioni 215.8 kulipa madeni mengine mbalimbali. Alisema Sh. milioni 103.4 zilitumika kwa ajili ya uendeshaji na sh. milioni 696 zilitumika kwa shughuli za maendeleo. HEBU FIKIRIA KUNA KULIPA MADENI 73.8 MIL NA MIL 215.8 KULIPA MADENI MENGINE MBALIMBALI!!!! - tofauti ni nini hapo?
lengo langu kutokea hewani ni kusisitiza kuwa mapato ya taifa kama hayatadhibitiwa basi maendeleo ni kwenye radio na luninga za wenzetu. japokuwa serekali ya Ben, japo ilisifika kwa ukusanyaji mkuu wa kodi lakini pia maendeleo hayakuonekana. lakini naye si alianza kwa kazi? mnakumbuka ile mambo ya milioni 900 zilizopotea akianza uongozi tu? pia serekali yetu na wananchi kama tusipojiwekea vipaumbele basi hela hata siku moja haitatosha. nakumbuka mwalimu wangu wa uchumi mwaka wa kwanza chuo kikuu alinifundisha kuwa uchumi ni kupanga rasilimali chache tulizonazo katika vipaumbele tulivyonavyo. si mwepesi kusahau mimi. je leo hii kufyatua dege http://www.darhotwire.com/dar/maoni/15002.html kwenda kutambika ni kitendo cha kushabikia kweli? suala lingine ni kuwa mbona hatupendi kuwajibika mambo kama haya yanapotokea? je kutambika ni kipaumbele cha taifa hadi ndege itumike? je zaidi ya darhotwire, mbona magazeti mengine hatuyasikii? tunamsaidia raisi kweli?
sasa hivi hapa makamu wa raisi wa afrika kusini yuko kwenye kiti moto kizito kuchukua ndege ya serekali kwenda UAE kwa mapumziko mwisho wa mwaka, na ni ya visiku vichache...mbaya zaidi alikuwa na mumewe pia ambaye alienda kufanya biashara ya macrane ambayo mama anadai kuwa ni kwa ajili ya taifa........kwa kweli sasa amebanwa na mjadala uko hapa http://www.mg.co.za/articlePage.aspx?articleid=261660&area=/breaking_news/breaking_news__national/ kwa kweli jana asubuhi niliuona kwenye TV mjadala mkali na wenye maana wa tume ya bunge Parliament's Joint Standing Committee on Public Accounts (Scopa) ukihusisha wanasiasa wa ndani na nje ya ANC wakimjadili huyu mama na safari yake. Public protector amekubali kuwa teyari ameishapata dili la kucheza naye....habari zaidi ziko mtandaoni.......
tunazungumzia Afrika kusini nchi yenye kipato kikubwa...inapata homa kwa hivyo vicenti....je tanzania ambayo hatuna kitu tuna haki gani ya kukaa kimya tukiambiwa mlitaka nikapande baiskeli???milioni kumi na laki sita (madawati ya shule nzima?) zinapotumika kutambika just like that??
mwandani samahani, huu sio mwendelezo wa ule mjadala wetu....bado nimebanwa lakini zilinipanda kidogo kuhusiana na vipaumbele!
alhamsiki!







