Thursday, February 17, 2011

UHUNI UTATUMALIZA WATANZANIA!

MAKALA hii ilitumwa kwa gazeti la mwanahalisi via halihalisi06@yahoo.com ikakosa responce, ni bora sasa tuiweke kwenye net ili tushirikishane!

Tukirejea mazungumzo yaliyofanywa na Jenerali Ulimwengu siku UDASA walipofanya kongamano la katiba pale mkurumah hall UDSM kinachoonekana kuisumbua Tanzania ni uhuni ambao kwa bahati mbaya (unfortunate) umelelewa katika ngazi za juu za serekali. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili kama ilivyonukuliwa tarehe 26 January 2011 katika tovuti (http://www.kamusiproject.org/en/lookup/sw?Word=uhuni) uhuni umepata majina mbalimbali kama vile vandalism (uharibifu), vagrancy, lawlessness+ disorderly conduct (kutofuata utaratibu), hooliganism, immorality (kutokuwa na maadili) moral decline (kuporomoka kwa maadili) na decadence (uovu).


Uongozi wa umma umekuwa ni ngazi ya watu kujipatia utajiri. Hii inajidhihirisha miongoni mwa maneno ya baadhi ya wanasiasa hao wakisema bila aibu kuwa walijitolea kuacha mambo mengi na kazi nzuri siku za nyuma ili watumikie vyama vyao. Ukiwatazama kwa matendo yao sasa hivi wakiwa kwenye madaraka utagundua kuwa walikuwa wanawekeza na kwamba sasa hivi wanapurura ili kufidia mapengo! Kuchuma kwa jasho ni jambo ya kawaida kwa maisha ya mwanadamu. Tunafanya kazi ili tuweze kumudu maisha yetu. Lakini kwa hawa wenzetu sio hivyo. Wanapurura kwa fujo hadi kujenga jamii ambayo sio endelevu. Unapopopoa embe changa unategemea kesho uje uzipate mbivu kweli? Je ina maana watoto tunaowazaa sasa hivi wasipate elimu bora? Wasipate huduma bora za afya kwa sababu wenye dhamana wameamua hivyo? Je waliotuachia nchi hii kweli pamoja na mazuri yoote walituambia tukitelekeze kizazi kipya? Baba yangu siku zote huwa ananiambia nimpe mtoto wangu malezi bora kama zawadi ya yeye kunilea mimi! Tunatakiwa tuwaachie watoto wetu zawadi na sio mateso!


Pale ambapo uongozi wa umma unamkataza mtu kufanya jambo moja, mfano wizi, na wote tunaelewa wizi ni mbaya, akaja mheshimiwa mmoja akafanya wizi, ilihali akijua kuwa anachofanya si sahihi huyo ni muhuni. Kama nafsi yako inakusuta wakati unatekeleza uhuni ambao kimsingi ukiukaji wa taratibu zilizopo au matarajio ya umma uliokuweka madarakani unakunja sura kidogo na unakuwa an awkward person. Hapa ndipo hata busara huyeyuka, na wananchi wako wakikuuliza basi wewe unawahi kuwasakizia polisi. Bahati mbaya sana hadi sasa hatujaweza kuwa na namna ya kuwabana wezi walio na vibali vya wapiga kura. Tuna TAKUKURU ambayo si huru. Changamoto iliyopo hapa sasa ni jinsi gani wahuni waliopewa dhamana waweza kuenguliwa katika dhamana walizonazo. Tumeona wahuni wakifanya mambo ya kihuni kasha wakapokelewa huko kwao kwa ngoma na sherehe!!


Kwa kiasi mkubwa mtaji wa wanasiasa watawala wetu umekuwa ni umasikini na ujinga uliokithiri miongoni mwa watanzania. Mazingira haya ambayo inawezekana kabisa kuwa yameundwa kwa makusudi na wakubwa zetu ndio yanawafanya wanyonge kuona samaki e wa leo ni bora kuliko wavu wa kuvulia kesho! Makusudi haya ni yanawafanya wakubwa hawa kuendelea kustahili heshima ya uhuni! Tatizo hili haliishi hapa tu na ni kubwa zaidi kwa wasomi ambao wengi wetu tuko kama fisi. Kwa wale waliosoma soma vihekaya hapo zamani watakumbuka hadithi ya mlevi mmoja aliyekuwa anatoka kilabuni. Kuna fisi mmoja alimwona mlevi huyu akitoka kilabuni akitembea akaanza kumfuata nyuma nyuma akitoka udenda ili mkono utakapoanguka tu basi auwahi akajipatie shibe yake. Fisi huyu alisikitika sana mlevi alipoingia ndani mwake na hakuna mkono ulioanguka. Wasomi wa sasa tuko hivyo. Tunajipendekeza kinafiki kwa wenye dhamana wan chi ili tuweze kupata upendeleo mmoja au mwingine. Hapa tumekuwa tayari kusema hata uongo ili tu mambo yetu yaende vyema. Tumesahau kuwa hata elimu tuliyo nayo imegharamiwa na wakulima na wafanyakazi wa nchi hii ambao wengi wao wanashindwa hata kugharamia matibabu yao. Tumewasaliti wakulima na wafanyakazi wa nchi hii. Tabia hii ya unafiki imejijenga sana miongoni mwetu na hata miongoni mwa maafisa wengi wa serekali ambao wako tayari kudanganya, kutumia taaluma zao kutoa ushauri potofu kwa sababu wanazozijua wao wenyewe na hata kukiuka taratibu za kazi alimradi tu wajipatie mradi wao na bwana mkubwa ajue na wao wamo. Jambo hili limejionyesha katika mikataba mbali mbali inayoitia taifa hasara, pale ambapo wataalamu tuliowapa heshima hiyo ya kutuwakilisha wanatugeuka na kukimbilia katika jukwaa mbali mbali kudai kuwa hasara hizi haziepukiki! Huu ni uhuni! Ni aibu kubwa sana unapoona pale wakuu wa polisi raia wanapokubali maagizo ya wanasiasa wahuni waliopoteza dira kwenda kujipa mamlaka ya kuingilia maandamano na kuua raia ambao hawana hatia! Polisi hapa hawawezi kujitakasa na kujiita kuwa sio wahuni! Mbaya zaidi ni pale polisi hawa hawa ambao wanalipwa na kununuliwa zana za kazi na raia wanyonge wa taifa hili wanapoacha kuomba msamaha walau hata kujuta na kujifunza kwa yaliyotokea, wakazana kuhariri mikanda ili kuuhadaa umaa kinyume cha hali halisi. Huu ni uhuni zaidi! Wanasahau kuwa kwa kufanya hivyo wameendelea kutumia rasilimali za taifa ambazo zingeweza kuleta faida zingetumika vinginevyo!

Wakati umefika sasa wasomi tuseme tusimame na tuseme ukweli ili kunusuru taifa letu linaloangamia kwa kasi. Je ni nani alifanya upembuzi wa hasara na faida (cost benefit analysis) akasema kubinafsisha shamba kule Mbarali kunalipa kuliko kuwakabidhi wananchi wajilimie mpunga wao? Je alitafakari kuwa inawezekana kuwa sehemu kubwa ya mpunga huo unapolimwa na mwananchi wa kawaida unapatikana zaidi kama chakula kwa wananchi wa kawaida? Je alitafakari kuwa masikini wakulima wale wakiwa na ardhi yao wanaweza kuwekeza nguvu zao wakajiuzia mchele wakala na ziada wakauza? Sasa wawekeze wapi? Waende kituo cha uwekezaji cha taifa (TIC) wakatafute pahala pa kuwekeza au soko la hisa la Dar es salaam (DSE) wakanunue hisa huko?. Je aliyefanya tathmini hii aliangalia utaifa au alijali maslahi binafsi zaidi? Matokeo yake ni moto wa wananchi kudai chao hadi kufikia pahala pa polisi wanadiriki kumpiga risasi mkulima anayetetea maslahi juu ya ardhi iliyozika vizazi na vizazi vya babu zake? Damu ya mwananchi huyu iko mikononi mwa nani? Mhuni mwanasiasa? Mhuni msomi au Mhuni polisi? Tumeona tena huko Rufiji. Mara hii wananchi wamekataa. Tunaowakabidhi rasilimali zetu ni wawekezaji au majambazi? Uhuni utatumaliza Watanzania!

Tazama tena, hili la shule za kata. Meneja kampeni wa mgombea mmoja wa uraisi alidiriki kusema kuwa suala la ada kwa wanafunzi sio tatizo kwani serekali inatoza shilingi ishirini elfu tu. Je wote tujiulize, je yeye mheshimiwa anapeleka mtoto kwenye shule ya shilingi ishirini elfu? Nini thamani halisi ya shilingi ishirini elfu inapokuja suala la elimu? Ni bora elimu au elimu bora? Leo hii tunaona watanzania walio wengi bila kujali unyonge tulionao tunakimbizana tutafute mamilioni kwenda kusomesha watoto ili angalau wanaporudi nyumbani uone matokeo. Ugharamiaji huu wa elimu unapelekea watu wengi kushindwa kukidhi mahitaji yao ya msingi na hata ya kimaendeleo. Je vijisenti vinavyochezewa chezewa na wakubwa haviwezi kuboresha mazingira hivyo kuwapunguzia makali wananchi. Je mheshimiwa wakati anaongea hilo la kuwa ada ya elimu ni inayowezekana kumudu alisema tu kwa sababu ana mdomo au aliona alilolizungumza ni halali? – je lilipata kibali cha ndani ya moyo wake au ilibidi aikane nafsi yake? Je huu nao sio uhuni? Tunapokazana kukimbilia kulipa DOWANS ambayo uwepo wake ni wa kihuni, na kuwaacha watoto wa wakulima na wafanyakazi kama msichana Salome Samburu wa Chuo Kikuu Makumira akizimia kwa kukosa mkopo wa masomo tunawezaje kujiita kuwa sisi sio wahuni? Je hatujui kuwa kodi inayolipwa na Mzee Samburu ndiyo inayetuwezesha kutimka huku na huko kwenye madhifa tukitumia maV8 tukipigwa na kiyoyozi? Tunasikia raha gani wanafunzi wa kike wanakiri hadharani kuwa bora wao wanajiuza na kufanya maisha lakini sio wenzao wa kiume ambao hawana pa kujiuza? Je vipaumbele vya taifa vinavyowekwa juu chini chini juu havitutunukii shahada za uhuni?

Kuna maswali ambayo hadi sasa ninajiuliza, na nina imani kizazi kipya kitahitaji majibu tu kama sio kwa wakubwa wa sasa basi itakuwa kwetu. Je ni nini kiliua mashirika mazuri aliyoyaanzisha mwalimu? Je ni nini kiliua vyama vya ushirika? Je tunayoyasikia kuhusu DOWANS na TANESCO ni mwendelezo wa yale yale? Hivi kariburi tumesikia kuwa vyama vya ushirika vitafufuliwa tena, tunajipanga vipi kutorudia tulikotoka? Je kwa mwendo huu uwekezaji wa taifa katika maeneo mbali mbali kama Kilimo Kwanza ni salama kiasi gani? Je Kilimo Kwanza na vyama vya ushirika sio DOWANS ya kesho na keshokutwa? Lahaula, kuna mradi wa vitambulisho vya taifa! Majengo na miundombinu inayoinuka hapa na pale, Je nayo haiko kwenye mtiririko huo huo? Mara zote historia hutumika kujifunza sijui kama tunafanya hivyo. Inavyooneka kabisa tukiendelea kwa mwendo huu Tanzania inaweza kuwekwa katika kundi la nchi zisizotaka kuendelea. Kimsingi tumefika mahali ambapo kila uwekezaji wa taifa unahisiwa kuleta maumivu kwa wananchi! Lakini hadi sasa hivi ni nani amewajibika kwa uhuni huu unaoendelea? Ni nani amewajibishwa kutokana na uuaji wa vyama vya ushirika? Mashirika ya umma? Ujambazi unaofanyika kwa kupitia kampuni zisizo na vichwa wala miguu mfano Meremeta, Tanpower na mengineyo? Tunasema majibu wa haya yote yanatakiwa!! Ukweli ni kwamba jamii ya kizazi kinachokuja ambacho kitakuwa kimepoteza fursa kadiri miaka inavyozidi kwenda kitakuja kufurusha watu na mawe. Ni kizazi kinachotaka majibu ya kueleweka kwa maswali watayoyauliza. Sio haya majibu ya kihuni kihuni!


Je dhana ya uwajibikaji kutokana na uhuni au yatokanayo na matendo ya uhuni ipo? Na kama haipo ni kwanini? Hebu tujiulize, tulisikia mahakama ikiomba mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kusikiliza kesi za uchaguzi. Hili halipaswi kuishia hapo tu. Je wasimamizi wa chaguzi waliyehusika na kuharibu chaguzi mbalimbali wanafidia vipi hasara waliyosababisha? Kwa maslahi ya nani unamtaja kuwa Fulani kashinda na sio mshindi halisi? Tuje kwa hili la Arusha. Kuna kila aina ya dalili kuwa uchaguzi wa Meya ulifanywa bila kufuata utaratibu. Hii ina maana kuwa kila aliyeliwezesha na kulibariki zoezi hilo ni muhuni. Uhuni huu ndio umepelekea Geneva ya Africa kukumbwa na machafuko siku za karibuni. Aliyechukua madaraka ya umeya kwa njia sio stahili ni muhuni pia. Aliyeleta polisi kuua raia ni muhuni zaidi. Cha msingi hapa ni kwamba je, ni hatua gani zinachukuliwa dhini ya wahuni walioichafua Geneva ya Africa? Kimsingi hapa dhana nzima ya uongozi bora inakuwa imekiukwa. Utawala bora ambao ndio msingi wa maendeleo umekiukwa kwa kuweka kiongozi ambaye sio watu walimtaka. Hii ina maana kwamba kitendo cha bwana Gaudensia kula kiyoyozi kwa miaka mitano kinagharamiwa na kurudi nyuma kwa maendeleo ya jiji la Arusha. Kwa kuzingatia dhana ya kwamba Tanzania ni nchi isiyotaka kuendelea, hili lawezekana; tena mia kwa mia. Mzee Lowassa kama mkazi wa Arusha aliliona hilo mapema na athari zake, ila wenzake ambao hawafikirii kuwa dhana nzima ya kupeleka uongozi kwa watu (devolution by decentralization) ni chachu ya maendeleo wakaendeleza ubabe. Inashangaza sana kwani watu hawa ambao wanaielewa dhana nzima ya utawala bora wa watu kama chombo muhimu cha watu kujiletea maendeleo, walikuwa kwenye nafasi za uongozi wakati Mwalimu anaihubiri na kuitekeleza! Je watu hawa ambao wanakinzana na nafsi zao wanatushawishi vipi kuwa wao si wahuni?

Wamemfurusha Spika wa bunge la tisa la Jamhuri! Mzee Samuel Sitta ambaye rekodi yake ya uendeshaji bunge ilikuwa bora kabisa! Huyu alikuwa hazina kubwa ya CCM na watanzania kwa ujumla. Walimuacha achukue fomu, halafu wakasema wanaume hapana! Hatukatai kuwa wanawake wanaweza, na mara nyingine huwa wanayamudu majukumu yao vizuri zaidi kuliko sie wanaume! Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, huu ulikuwa uhuni wa hali ya juu!. Ukiukaji wa taratibu unaweza kuwa ni utaratibu unaokubalika kwa kundi lingine. Kwa hili lakini siwezi kulisemea sana kwani wanajua wanavyokubaliana kwenye chama chao! Na ndio maana pengine hata Mzee Sita bado yuko kwenye chama hicho! Hata hivyo alipokuwa Spika huwa anatuhusu watanzania wote hivyo hata sisi wengine tumeugua kwa hilo!

Tumesoma kwenye magazeti wakati wa dakika za lala salama kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, jinsi mtu aliyewahi kukiri kuwa hana imani ya dini na kuaminiwa kama mshauri wa siasa wa mkuu wa nchi akiwaangukia maimamu wa misikiti kule morogoro kuwa wamchague mgombea wake kwa sababu kuna ombwe na dini linatumika na wagombea wengine! Sisi tunaomfahamu Mzee Kingunge tangu utoto wetu, kufikia pahala tukamwita mtu yeyote aliyeiva na kuenea kisiasa kuwa ni kingunge tulishtushwa sana na hili! Tulipata wasiwasi kuwa pengine mzee wetu huyu ameanza kupoteza kumbukumbu kwani katika umri wake huu asingeweza kudiriki kuchafua historia yake aliyoijenga miaka mingi katika Nyanja za siasa! Na kama ana kumbukumbu kamili basi kuna hatari kubwa kuwa ameingia kwenye kundi la wahuni! Falsafa ya udini ambayo imewashwa, inazungumzwa na kupepelewa na viongozi tuliowakabidhi inchi yetu haionekani miongoni mwetu sisi raia wa kawaida! Ninachelea kutamka wazi kuwa kila anayehubiri kuwa Tanzania kuna udini ni mhuni mkubwa na anapaswa kuuomba radhi umma wa watanzania kwa kutaka kukifanya kizazi kipya kiwe wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe!

Je ni kwanini hadi leo hii mgombea binafsi hakubaliwi? Ni kwa nini mtu apate ridhaa ya chama ili aweze kugombea? Japo ni woga wa bure lakini upande mmoja kulikuwa na mantiki kuwa mtu awekwe na kikundi ambacho nia na madhumuni yake baada ya kukamata dola yawe bayana. Kuwepo na mkataba wa uongozi wa nchi. Kukataa kuungwa mkono na kundi mhimili la chama chako kuna maana gani? Ujumbe wa kukataa kura za wafanyakazi kina tafsiri gani? Je si kwa sababu gani ilionekana kuwa ni muhimu kuwa na chata ya jembe na nyundo kwenye chata ya chama chako? Tumevaa kofia hizi na kanga hizi! Lakini je si ni wakati wa kubadilisha chata hiyo na kuweka viashiria kuwa chama hiki sasa ni cha kundi tofauti na tulivyodhani hapo mwanzo? Je tupo kwa ajili ya mkulima na mfanyakazi wa taifa hili? Ambaye sasa anaelekea kushindwa kumudu hata mlo mmoja kwa siku? Ambaye ana mtoto mwenye akili lakini chuo kinapofunguliwa hawezi hata kupewa nauli ya kurudia chuo? Anayekosa shilingi mia tano ya kununua panado akipata homa? Lakini anayelilisha taifa hili chakula miaka nenda miaka rudi, tukijua fika kuwa kuwa hatununui mazao yake kwa bei stahili hivyo hatumtendei haki? Kwa nini tusichore picha za almasi, na maghorofa kwenye kofia badala ya jembe na nyundo? Je ndio mabadiliko ya kimuundo au bado ni mwendelezo wa dhana ya uhuni – kutenda kinyume cha makubaliano?

Tujitafakari, tuchukue hatua, tena sasa kabla hatujachelea uhuni utatumaliza waTanzania!

Labels:

10 Comments:

At 1:24 AM, Anonymous Profee said...

Picture kidogo basi!

 
At 5:36 PM, Anonymous Anonymous said...

Decide to be a good person who will not be evil.
Inherent in the offer of clone hosting is a clue:::"Earn" by hurting others. This violates this vow, causing people to incurr evil, and the clue you need to avoid it. Sadly, as young people too many are still corrupted, still unenlightened and make the mistake when offered.
Only innocent pure children ascend into heaven, while evil is relegated to entering clone hosting, where they are reincarnated as lesser life forms. One day the Christian Rapture will be used as a "consolation prize", and usher in the era of compensation according to the Bible:::1000 years with Jesus on Earth.
Everlasting life with Jesus, but only for true believers:::Placement to suffer on the next Planet Earth punishment for worshipping a false god.

"Some people are evil." This is the gods fulfilling people's history by pushing them into that legacy. This is the gods accepting culpability and blame with their participation.
As we devolve and approach The End the gods transition to temptation, deceiving them into thinking they are "earning", allowing them to wash their hands of culpability. As this occurrs for more of us in society the gods are preparing for the Apocalypse, for when The End comes the gods will not be to blame for the result.
The disfavored think the opposite, that now that they are participating they have favor, and they will live forever because of it.

1.14
9:20a
Talk of Republicans unwillingness to raise the debt ceiling. They insist on spending cuts.
As inefficent as government has been allowed to become perhaps we should begin with the size of government and look to their own support staff. Sacrifice needs to be made by all. I am concerned there is nepotism and favoritism occurring in these support jobs, and the size gets out of hand because of it. I would expect these Republicans would not be willing to look within their own offices.
Federal and state governments is very much like the farmer and his water allocation:::To continue to achieve increasing allocations they would rather discharge the water rather than report underuse.
Perhaps if I worked at the Department of Education in Pleasant Hill some progress could have been made, a framework allowed by this preditory DM. But watching them instruct the clone host fakes in the Federal government to hold out and force the consservative Democrat Obama to look bad illustrates teh Antients have made up their minds and intend to force it.

The gods may share some values of the conservatives (mostly good, a little evil), with the exception of capitalism, warmongering and environmental degredation, but they also share in the economic degredation of the conservatives which will bring the United States to bankrupcy and anarchy. It initiated with Ronald Reagan taking the National Debt from $1T to $6T.
And me, the hundred billion dollar man, will have to meekly ask for a nice apartment (conservative timeshare dream).
As long as the gods have this vested interest of the Situation they are calling the shots. They order all proceedings to ensure they get what they want. This is not to say they will transistion when it is over, but I suspect this final absolution of culpability is necessary for them to completely wash their hands of Earth in preparation for the Apocalypse.

The gods gave you AIDS in Africa to correct your promiscuous sexual behavior, just as they did with the homosexuals in the United States in the 1980s. They used those who destroyed life on Planet Earth to do their legwork, as they did with most other important elements. This way they managed their culpbaility, are not to blame and can walk away cleanly.

 
At 10:22 AM, Anonymous obat bius said...

I 'm so glad you could come across this site ,
and we hope to establish good relations with you.
greetings from me ( Apotikobatbius.com ).
obat bius
obat tidur
apotik obat tidur

obat kuat
obat perangsang wanita

jual obat bius
jual obat tidur
apotik obat bius

 
At 10:24 AM, Anonymous Boneka Full Body said...

thanks you

 
At 1:26 PM, Anonymous Vimax Original Solusi Pria Perkasa said...artikelnya sangat membantu gan thanks for sharing :)

 
At 2:12 PM, Anonymous Vimax Canada said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you

 
At 1:12 PM, Anonymous obat vimax said...

Thanx for sharing ilike your book

 
At 7:05 AM, Anonymous Vimax Canada said...

thanks you for information

 
At 7:05 AM, Anonymous Selaput Dara Buatan said...

i like it this blog, thanks for saharing

 
At 5:06 AM, Blogger poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home